Jumatano jeshi la Congo lilizuia wafuasi wa dhehebu moja kufanya maandamano dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa, Monusco, kwenye mji wa Goma. Awali watu 10 waliripotiwa kufa baada ya wanajeshi hao kuvamia kituo cha radio pamoja na nyumba ya ibada, kulingana na vyanzo vya mji huo, wakati askari mmoja akiripotiwa kuchomwa na umma wakati wa ghasia hizo.
Kundi la wanaharakati wa demokrasia la LUCHA, Alhamisi limesema kwamba watu waliokufa ni karibu 50, wakati nyaraka ya kijeshi iliyoonyeshwa AFP ikiongeza kwamba kando na wale 48 waliokufa, wengine 75 walijeruhiwa. Ujumbe wa walinda amani wa UN nchini Congo ni mojawapo ya mikubwa zaidi ulimwenguni wakati ukigharimu takriban dola bilioni 1 za kimarekani kila mwaka.
Forum