Waangalizi wa UN awali waliripoti kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba vikosi vya Mali pamoja na washirika wake wa kigeni wanaoaminika kuwa mamluki ya kundi la Wagner kutoka Russia, wanadhulumu wanawake huku pia wakikiuka haki nyingine za binadamu, ili kueneza hofu.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, wanachama 13 wa baraza hilo walipiga kura kuunga mkono pendekezo la Ufaransa na Umoja wa Falme za Kiarabu la kuongeza muda wa vikwazo vya Umoja wa Mataifa, pamoja na uangalizi kwa mwaka mmoja zaidi.
Russia ilipiga kura ya kupinga wakati China ikisusia kura hiyo. Russia badala yake imependekeza kuongezwa muda wa vikwazo nchini Mali kwa mwaka mmoja, lakini timu ya uangalizi iondolewe. Naibu balozi wa Marekani kwenye UN Robert Wood ameambia baraza hilo kwamba Russia inapendekeza kuondolewa kwa timu ya uangalizi ili kuficha maovu ya Wagner nchini Mali.
Forum