Wamesema mtu aliyejitoa muhanga alikusudia kuulipua msafara wa maafisa wa usalama katika mji mkuu wa mkoa wa Pul-e-Alam.
Msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid alikanusha mara moja kuhusika na tukio hilo, akisema wapiganaji wao walikuwa hawahusiki kabisa na shambulizi hilo, ambalo limetokea saa kadha kabla ya makubaliano ya Taliban ya kusitisha mapigano kwa siku tatu wa Eid kuanza kutekelezwa.
The festivities started Friday and the Afghan government ordered security forces to cease operations against the insurgents.
Sherehe za Eid zimeanza Ijumaa na serikali ya Afghanistan imeagiza wanajeshi wake kusitisha operesheni zote dhidi waasi.
Baada ya sala maalum ya siku ya Eid Ijumaa asubuhi, Rais Ashraf Ghani alitangaza katika hotuba yake iliorushwa kwa njia yakwamba televisheni serikali yake inashughulikia kuwaachia huru kiasi cha wafungwa 5,000 Wataliban ili kubadilishana na mateka 1,000 wa vikosi vya usalama vya Afghanistan kutoka mikononi mwa waasi
Chini ya makubaliano ya kubadilisha wafungwa yalioainishwa katika mkataba wa amani kati ya Marekani na Taliban.
Ghani amesema, hata hivyo, yeye hanaruhusa ya kuwaachia wafungwa hao kwa uamuzi wake peke yake.
Amesema mkutano maalum wa wazee unaojulikana kama jirga, au baraza la watunga sheria, litaitishwa kufanya uamuzi wa kuwaachia wafungwa waliosalia ili mazungumzo ya makundi mbalimbali ya Afghanistan yaweze kuanza.