Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:12

Shamrashamra za Eid-el-Fitr baadhi ya nchi za kwamishwa na karantini


Waislamu katika mskiti mjini Sidoarjo, Java Mashariki, Indonesia wakati wa sala ya Eid al-Fitr
Waislamu katika mskiti mjini Sidoarjo, Java Mashariki, Indonesia wakati wa sala ya Eid al-Fitr

Waislam katika sehemu mbali mbali duniani wameanza kuadhimisha sikukuu ya Eid al-Fitr isiyokuwa na shamrashamra Jumapili, wengi wakiwa chini ya amri ya kutotoka nje.

Hata hivyo kulegezwa kwa masharti katika baadhi ya nchi kunatoa afueni kwa waumini katika baadhi ya nchi pamoja na kuwepo hofu ya maambukizo ya hali ya juu ya virusi vya corona.

Sikukuu ya siku tatu, inayoadhimisha kumalizika kwa mwezi mtufuku wa Ramadhan, kwa kawaida inasheherekewa misikitini, karamu katika familia na ununuzi wa nguo mpya, zawadi na kupeana vyakula vitamu.

Virusi vya corona

Lakini mwaka huu, sherehe hizo zimeghubikwa na kuenea kwa virusi vya corona, ambapo nchi nyingi zimeweka masharti makali ya kutotoka nje baada ya kulegeza masharti hayo wakati wa mwezi wa Ramadhan iliyopelekea mlipuko mkubwa wa maambukizi.

Ikiathiri hata zaidi sherehe za kidini, katika nchi nyingi hasa Mashariki ya Kati – kutoka Saudi Arabia mpaka Misri, Uturuki na Syria –nchi hizi zimekataza ibada zenye mikusanyiko, wakati wa sherehe hizi, ili kupunguza kuenea kwa ugonjwa huo.

Makka na Madina

Saudi Arabia, ambayo ndio kitovu cha maeneo matakatifu ya Uislam, ilianza kutekeleza amri ya kutotoka nje saa 24 kwa siku tano, kuanzia Jumamosi baada ya maambukizi kuongezeka mara nne zaidi tangu kuanza kwa mwezi wa Ramadhan na kufikia zaidi ya wagongwa 70,000 – idadi ya juu kuliko zote katika nchi za Ghuba.

Msikiti Mkuu wa Makka umekuwa na waumini wachache wanaohudhuria ibada tangu mwezi Machi, ambapo kwa ajabu eneo la Kaaba tukufu ambalo kawaida huzungukwa na waumini kila wakati, kwa mara ya kwanza likiwa halina watu – Kaaba ambayo ni ya mraba ambapo waumini hufanya ibada zao.

Lakini siku ya Jumapili, Imam mmoja alisimama katika membari wakati maafisa wa usalama, baadhi yao wakivalia barakoa, walikuwa wamesimama kati kati ya mistari ya waumini waliokusanyika mbele ya Kaaba kutekeleza ibada ya Eid—misala yao ikiwa imetenganishwa ili kutokaribiana.

Msikiti wa Al-Aqsa

Huko katika msikiti wa Al-Aqsa, Jerusalem, eneo la tatu takatifu la Uislam baada ya Makka na Madina, sala ya Eid haikuruhusiwa ndani ya msikiti huo, pamoja na kuwa eneo hilo lilitarajiwa kufunguliwa tena baada ya sikukuu ya Eid.

Wakati wa alfajiri, mapambano yalitokea kati ya maafisa wa usalama wa Israeli na waumini waliokuwa wamekusanyika nje ya msikiti huo. Hata hivyo Sala ya Eid hatimaye ilifanyika nje, mpiga picha wa shirika la habari la AFP alisema.

Wanawake wakipalestina wasali kwenye uwa wa mskiti wa al-Aqsa, Mji wa Kale wa Jerusalem
Wanawake wakipalestina wasali kwenye uwa wa mskiti wa al-Aqsa, Mji wa Kale wa Jerusalem

Huko Gaza, serikali ya Hamas iliruhusu sala kufanyika miskitini pamoja na kuwepo kifo cha kwanza cha mgonjwa wa virusi vya corona Jumamosi, lakini waumini wengi wao walikuwa wamevalia barakoa na waliweka misala yao hatua kadhaa ili kutosogeleana wakati wa ibada hiyo.

Akizungumza na shirika la habari la AFP Akram Taher mumini moja amesema “Sherehe za Eid hazifani manmo wakati huu wa hali ya janga la corona – watu wanahisia ya kua na hofu”

Bara la Asia

Waislam katika bara la Asia – kutoka Indonesia hadi Pakistan, Malaysia na Afghanistan – wamekusanyika katika masoko katika shamrashamra za manunuzi ya sikukuu, wakikiuka muongozo wa kudhibiti virusi vya corona na wakati mwengine polisi wakijaribu kutawanya mikusanyiko ya makundi makubwa.

“Kwa kipindi cha miezi miwili watoto wangu wamekuwa ndani,” amesema Ishrat Jahan, mama mwenye watoto wanne katika soko lenye harakati huko katika mji wa Rawalpindi nchini Pakistan.

“Karamu hii ni kwa ajili ya watoto, na kama hawataweza kusheherekea Eid kwa kuvaa nguo mpya, hakuna sababu ya sisi kufanya kazi kwa bidii mwaka mzima.”

Indonesia

Waislamu wasofuata masharti ya kutokaribiana katika mskiti wa Medan, Sumatra kaskazini, Indonesia
Waislamu wasofuata masharti ya kutokaribiana katika mskiti wa Medan, Sumatra kaskazini, Indonesia

Nchini Indonesia – taifa lenye Waislam wengi zaidi duniani – watu wamehiari kuwatumia walanguzi na hati bandia za kusafiri ili kukwepa amri za kutotoka nje kwa ajili ya kusafiri wakati wa kumalizika Ramadhan jambo ambalo linaweza kuongeza maambukizo.

Katika jimbo la wahafidhina la Aceh, makundi makubwa ya watu walikusanyika kufanya ibada ambapo wachache walivalia barakoa na wachache walisali bila ya kukaribiana, na msikiti mkuu wa Baiturrahman katika makao makuu ya jimbo hilo lilifurika watu.

“Nilikuwa na hofu kusali katika hali kama hiyo, lakini kama Muislam, niwajibu wangu kutekeleza ibada ya Eid kwa jamaa kama njia ya kumshukuru Allah,” mmoja wa wale waliohudhuria ibada hiyo aliiambia AFP.

Mashariki ya Kati

Idadi ya vifo kutokana na COVID-19 Mashariki ya Kati na Asia imekuwa iko chini kuliko Ulaya na Marekani, lakini maambukizo yanaongezeka, na kusababisha hofu ya virusi hivyo vinaweza kufanya mifumo ya afya ambayo haipewi fedha za kutosha kuelemewa.

Watt watembezwa kwa gari la mkokoteni latina mui wa Idlib Syria haiku ya Eid al-Fitr
Watt watembezwa kwa gari la mkokoteni latina mui wa Idlib Syria haiku ya Eid al-Fitr

Iran

Iran, ambayo imepitia mlipuko wenye vifo vingi katika Mashariki ya Kati, imewataka raia wake kuepuka kusafiri wakati wa Eid wakati ikipambana kudhibiti kiwango cha maambukizo nchini humo.

Waziri wa Afya Saeed Namaki amesema nchi hiyo imejikita kwa nguvu zote kuzuia “maambukizo mapya ya ugonjwa huo” yanayo sababishwa na watu “ ambao hawaheshimu kanuni za afya”.

XS
SM
MD
LG