Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:21

WHO yatahadharisha vifo zaidi barani Afrika iwapo serikali hazitachukuwa hatua


Mwanamke na mtoto wake wakimsikiliza mfanyakazi wa afya akieleza mchakato wa kuchukuwa vipimo vya COVID-19 , Johannesburg, Afrika Kusini.
Mwanamke na mtoto wake wakimsikiliza mfanyakazi wa afya akieleza mchakato wa kuchukuwa vipimo vya COVID-19 , Johannesburg, Afrika Kusini.

Shirika la Afya Duniani (WHO) Ijumaa limeonya kuwa watu 190,000 wanaweza kupoteza maisha mwaka 2020 barani Africa, iwapo serikali zitashindwa kudhibiti maambukizi ya virus vya corona.

WHO yatahadharisha vifo zaidi barani Afrika iwapo serikali hazitachukuwa hatua.

Shirika hilo limetaja utafiti mpya uliyofanywa na ofisi yake Brazzaville uliogundua kuwa kati ya watu 83,000 na 190,000 wanaweza kufa na wengine milioni 29 hadi 44 wataambukizwa katika kipindi hicho.

Utafiti huo umetolewa ukizingatia vigezo vya utabiri wa maambukizo na inaangaza katika nchi 47 zenye idadi ya watu bilioni 1, WHO imesema katika taarifa yake.

Wataalam wameendelea kuonya kuwa Afrika hasa iko katika hatari ya mlipuko wa maambukizo ya COVID-19, kwa sababu ya mifumo duni ya afya, kiwango cha juu cha umaskini, migogoro mbalimbali ya kivita, na uthibitisho wa kuwepo mazingira wezeshi ya maambukizo ya magonjwa ya milipuko.

Lakini maambukizo ya virusi yamekuwa yakienea polepole barani humo, ambapo hadi sasa haijafikia idadi kubwa ya maambukizo na vifo vilivyotokea Ulaya, Marekani na sehemu nyingine.

“Vigezo hivyo vinatabiri kuwepo maambukizi ya polepole, watu wenye umri mdogo ambao wanamagonjwa sugu na kiwango cha chini cha vifo ukilinganisha na kile kilichoshuhudiwa katika nchi zilizoathiriwa zaidi sehemu zilizobakia ulimwenguni,” taarifa hiyo ya WHO imeeleza.

“Idadi ndogo ya maambukizo, ni kielelezo cha mlipuko huo kuendelea kwa miaka mingi.”

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC

XS
SM
MD
LG