Hatua hiyo imekuja baada ya kujiridhisha kupungua kwa maambukizi ya COVID-19 nchini humo.
Akizungumza Katika hafla ya kuwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, Rais Magufuli ameeleza kuwa licha ya kuwepo kwa COVID-19, lazima wanafunzi waendelee na masomo na maisha mengine yaendelee.
Kwa wanafunzi wa madarasa ya chini, Rais Magufuli amesema kurejea kwao shuleni kutategemea na hali ya maambukizi itakavyokuwa katika siku za usoni.
Aidha, amezitaka wizara za elimu na fedha kuhakikisha zinaweka mazingira yote sawa kwa wanafunzi kuanza masomo ikiwemo fedha za mikopo ya elimu kwa wanafunzi wa vyuo pamoja na mazingira wezeshi, katika kipindi cha siku tisa zilizobaki kabla ya shule kufunguliwa kwa wanafunzi wa kidato cha sita kuendelea na masomo pamoja na mitihani yao ya kumaliza elimu ya sekondari.
Rais Magufuli pia ametangaza kufungua shughuli za michezo hususan ligi kuu za soka nchini humo huku akitaka tahadhari zote za kujingika na Covid 19 zizingatiwe.
Imetayarishwa na Mwandishi wetu Iddi Uwesu, Tanzania.