Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:05

Sikukuu ya Eid na Ibada ya Hijja zaadhimishwa kwa kuchukuwa tahadhari


Mahujaji wakiwa katika msikiti wa Makka, Saudi Arabia wakizunguka Kaaba, Julai 31, 2020.
Mahujaji wakiwa katika msikiti wa Makka, Saudi Arabia wakizunguka Kaaba, Julai 31, 2020.

Leo ni Sikukuu ya Eid el Hajj kwa Waislam duniani. Mataifa mengi duniani yanaadhimisha sikukuu hii kwa kuchukua tahadhari ya kuepuka mikusanyiko na pia watu wanasheherekea katika familia zao. 

Wakati huohuo Mahujaji nchini Saudi Arabia wamemaliza kufanya ibada ya kuzunguka Al-Kaaba mara saba, kufuatia siku ya kwanza ya kumbukumbu ya ibada ya kurusha vijiwe kumpiga sheitani iliyofanyika Ijumaa ambayo pia ni sikukuu ya Eid el Hajj inayohusisha ibada ya kuchinja mnyama na watu kukusanyika misikitin kusali sala ya Eid.

Katika baadhi ya nchi Waislam wanasali majumbani na sehemu nyingine misikiti imeweka utaratibu maalum wa kuruhusu idadi ndogo tu kuhudhuria ibada hiyo.

Ikiwa ni sehemu ya ibada ya Hija kila mwaka, Waislam wanavaa nguo nyeupe kwa ajili ya kuonyesha umuhimu wa unadhifu, wanapiga vijiwe katika kuta kubwa ikiwa ni ishara ya kumfukuza shetani kabla ya kwenda kuzunguka Kaaba, ibada inayojulikana kama Tawaf, katika msikiti wa Makka.

Waislam hao waliokuwa wamevaa barakoa wanazunguka nyumba takatifu ya Kaaba – ni jiwe lililowekwa ambalo ni takatifu kuliko mawe yote katika Uislam.

Kaaba ndiko Waislam wote wanaelekea kwa ajili ya kufanya ibada kila siku.

Katika kuzunguka Kaaba wako katika makundi ya watu 50, kila mmoja akikaa mbali na mwenzie na wakiwa wameambatana na wataalam wa afya ambao wanaangalia mwenendo wao iwapo unafuata utaratibu wa afya uliowekwa.

Kwa mara ya kwanza katika zama hizi za leo, katikati ya juhudi zinazoendelea kujikinga na maambukizi ya COVID-19, Waislam nje ya Saudi Arabia hawakuweza kuhudhuria ibada ya Hijja.

Mwaka huu ibada ya hija imehudhuriwa na watu wapatao 1,000 ambao wanaishi Saudi Arabia, asilimia 70 kati yao ni wakazi wageni wanaofanya kazi katika mamlaka ya Saudi Arabia.

XS
SM
MD
LG