Kupitia idara inayofuatilia ufadhili haramu wa makundi ya kigaidi TFTC hapa Marekani kwa ushiriikiano na mataifa ya ghuba ya kiarabu wameweza kukomesha ufadhili huo hasa kwenye eneo la mashariki ya kati na duniani kwa jumla. Nchi za Saudi Arabia, Bahrain, Kuwait, Oman. Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu pamoja na Marekani zimeweza kushihrikiana katika kutoa taarifa za kipelelezi za kifedha zinazoweza kuwa tishio kwa usalama wa taifa kwa kila moja wao.
Tangu kubuniwa kwa TFTC mwaka 2017 zaidi ya watu pamoja na makundi 60 yanayojihusisha na shuguli za kigaidi kote ulimwenguni wamedhibitiwa. Makuundi yaliolengwa ni ISIS pamoja na washirika wake kama al Qaida, Islamic Revolutionary Guard Corps, Hizballah kutoka Lebanon na Taliban miongoni mwa mengine.
Hivi karibuni TFTC iliweka vikwazo kwa watu 6 pamoja na makundi yanayoshirikiana na ISIS ikiwa juhudi zake za kuvunja ufadhili wa operesheni za kundi hilo kote ulimwenguni. Vikwazo hivyo vinalenga biashara zinazotoa huduma za kifedha nchini Syria zikiwemo la Haram Exchange, Tawasul na al Khalidi Exchange pamoja na watu binafsi kama vile Abd al Rahman Ali Husayn al Ahmad al Rawi pamoja na kundi lenye makao yake Afghanistan la Nejaat Social Welfare Organization akiwemo mkurugenzi wake Sayed Habib Ahmad Khan. Awali makundi hayo yalikuwa yamewekewa vikwazo na Marekani kupitia amri ya kiutendaji nambari 13224.
Mali zote au shuguli kutoka kwa makundi au watu waliotajwa lazima yazuiliwe kuingia hapa Marekani au ushirikiano wowote na watu wa marekani na ripoti lazima zifikishwe kwa idara inayoratibu mali zilizowekezwa nje ya nchi OFAC.
Waziri wa fedha wa Marekani Steven Mnuchin ameangazia juhudi za TFTC katika kuvunja mitandao ya ufadhili wa kigaidi kote duniani. TFTC imeimarisha ushirikiano wa Marekani na washirika wake kutoka ghuba ya kiarabu katika kukabiliana na tishio la ugaidi pamoja na juhudi za pamoja za kuvunja mitandao ya kifedha inayofadhili shuguli hizo popote ilipo ulimwenguni.
Waziri wa mambo ya nje wa marekani Mike Pompeo katika taarifa ya hivi karibuni amesema kuwa vikwazo vilivyowekwa ni onyo la kutosha kwa watu na biashara zinazotoa au kunuia kutoa ufadhili kwa makundi ya kigaidi.
Hiyo ilikuwa tahariri ya sauti ya Amerika inayoelezea sera na msimamo wa serikali ya Marekani.