Rais Joe Biden wa Marekani anasema anataka kufufua ushirikiano na nchi za Afrika, kwa maslahi ya pande zote mbili, alipokua anafunga mkutano wake wa siku tatu pamoja na viongozi 49 wa Afrika.
Akizungumza katika kikao cha mwisho siku ya Alhamisi Rais Biden alitangaza kwamba atatembelea nchi za Afrika mwaka 2023 ili kusisitiza dhamira yake ya dhati ya kusiadia nchi za Afrika kuweza kuimarisha uchumi wao na uwekezaji wa pamoja na makampuni ya Marekani.
Kiongozi huyo alitangaza mlolongo wa misaada ya kuimarisha uchumi, kilimo na ujasirimali miongoni mwa vijana na wanawake. Zaidi ya hayo alitangaza msaada wa dharura kukabiliana na njaa barani humo.