Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 00:02

Marekani: Chuo Kikuu cha Howard chapata rais wa kwanza mwanamke Mweusi


Chuo Kikuu cha Howard
Chuo Kikuu cha Howard

Chuo kikuu cha Howard kimetangaza Alhamisi kwamba Claudine Gay atakuwa rais wa 30,  mtu mweusi wa kwanza na mwanamke wa pili kuongoza chuo hicho.

Claudine ambaye sasa ni mkuu wa chuo na mtalaamu wa demokrasia atakuwa rais julai mosi.

Anachukua nafasi ya Lawrence Bacow ambaye anajiuzulu na alisema anataka kutumia muda zaidi na familia yake.

Kwa uteuzi wa Gay, wanawake watawazidi wanaume kama wakuu vyuo vyenye hadhi ya juu Marekani . vyuo vikuu vya Dartmouth na Pennsylivania viliteuwa wanawake mapema mwaka huu, wakijiunga na Brown na Cornell, wakati Columbia Princetown na Yale zinaongozwa na wanaume .

Drew Faust alikuwa mwanamke wa kwanza kuwa rais wa Howard. Mwanahistoria wa Amerika kusini na vita vya wenyewe kwa wenyewe alijiuzulu mwaka 2018 baada ya miaka 11.

Claudine Gay, rais mtarajiwa wa chuo kikuu cha Howard: “ kwa hiyo wazazi wangu ni wahamiaji kutoka Haiti. Wamekuja marekani na kitu kidogo na kuingia chuoni wakati wanalea familia. Mama yangu alikuwa muuguzi na baba yangu alikuwa mhandisi na kilikuwa chuo cha mjini Newyok , ambapo walifanikiwa katika tasnia hizo. Chuo kilikuwa siku zote ni matarajio kwangu.”

Gay anaongeza kusema:“ kwa hiyo leo tuko katika wakati wa mabadiliko ya haraka ya kijamii, kisiasa, katika uchumi, teknolojia. Mawazo mengi sana ya kimsingi jinsi ulimwengu unavyofanya kazi na jinsi tunapaswa kuhusiana sisi kwa sisi yanajaribiwa na mara nyingine yanabadilika katika vichwa vyao.

Kuna imani ndogo katika taasisi za kila aina na mabadiliko jinsi watu wanavyoona. Kuna ufikiaji usio na mwisho wa habari lakini inazidi kuwa vigumu kujua cha kuamini. Kuna njia mpya za watu kusema ukweli wao bila kujali kama wanashikilia nyadhifa za madaraka."

XS
SM
MD
LG