Mwanidshi wa Sauti ya Amerika mjini Mombasa Salma Mohamed ametembelea kituo kimoja cha kuwashughulikia watoto wanaogua utindio wa ubongo yaani cerebral Palsy na kutuandalia ripoti ifuatayo.
Kurunzi ni kituo cha afya ya viungo kwa watoto wanaoishi na utindio wa Ubongo maarufu cerebral palsy katika kitongoji kimoja mjini Mombasa.
Hapa watoto hao wenye ulemavu huo hufanyiwa matibabu ya kunyoosha mwili na viungo kama njia moja ya kuhakikisha miili yao inasalia katika hali nzuri. Ingawa kurunzi ni zahanati ya watoto wa Cerebral Palsy, hii pia ni sehemu maalum kwa wanawake kupata usaidizi wa kihisia na kimawazo.
Forum