Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 00:27

Rais wa Jamhuri ya Congo apongeza mafanikio ya Mkutano wa Viongozi wa Marekani na Afrika


Rais Denis Sassou N'Guesso
Rais Denis Sassou N'Guesso

Rais wa Jamhuri ya Congo, Denis Sassou-Nguesso anasema maendeleo makubwa yamepatikana katika mkutano wa mwaka huu wa  viongozi wa Marekani na Afrika uliofanyika Washington.

Nguesso ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ngazi ya juu ya Umoja wa Afrika kwa Libya ametaka dunia ielekeze macho yake katika kusuluhisha mzozo wa kisiasa nchini Libya.

Wiki iliyopita, Rais wa Jamhuri ya Congo, Nguesso alihudhuria mkutano wa pili wa viongozi wa Marekani na Afrika. Katika mahojiano maalum na Sauti ya Amerika (VOA) amesema kwamba wakati huu malengo yameelezewa kwa kina zaidi, ikiwa ni pamoja na kuisaidia Umoja wa Afroika kupata sauti kubwa zaidi katika Umoja wa Mataifa.

“Kwa mfano, Rais Biden alitangaza kwamba Umoja wa Afrika kwa hakika utakuwa mwanachama wa G-20. Naamini hii ni hatua ya dhairi ambayo tunaifurahia. Bwana Biden pia alitangaza kwamba katika miaka michache ijayo, Marekani itajihusisha katika Afrika kutafuta njia za sisi kuwa na nafasi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kama mwanachama wa kudumu,” amesema Nguesso.

Kundi la G-20 linajumuisha mataifa yaliyoendelea kiviwanda ulimenguni na uchumi unaonyanyukia. Afrika Kusini hivi sasa ni mwanachama pekee wa kiafrika katika kundi hilo.

Rais Joe Biden pia alisema kuwa utawala wake utatumia $ 55 bilioni kuzisaidia nchi zaz Afrika katika kipindi cha miaka mitatu ijayo. “Mkutano huu na Agenda ya 2063 ya Umoja wa Afrika, macho yetu yameelekezrwa katika musktabali wa baadaye,” aliongeza Biden.

Rais Joe Biden akiwa na viongozi wa Afrika katika picha ya pamoja.
Rais Joe Biden akiwa na viongozi wa Afrika katika picha ya pamoja.

Naye Rais Nguesso amesema hayo pia ni maendeleo muhimu, hasa wakati mjadala unaruhusiwa kuzungumzia vipaumbele vya Afrika. Rais Macky Sall, rais wa Umoja wa Afrika na viongozi wengine wote walisisitiza vipaumbele vya Afrika, iwe vinahusisana na miundo mbinu ya msingi, kuendeleza sekta ya kilimo, digitali, elimu, afya, na suala la nishati.”

White House ilisema itatumia $165 milioni kuimarisha demokrasia na utawala mzuri. Bado baadhi wamemkosoa Biden kwa kuwakaribisha viongozi ambao wako madarakani kwa muda mrefu sana. Maafisa wa Marekani wamesema viongozi wote wako katika maelewano mazuri Umoja wa Afrika na Marekani walipata ukaribisho.

“Demokrasiaz na utawala mzuri ni mchakato unaoendelea, na hata hivi leo kuna baadhi ya nchi Ulaya, kuna changamoto za uchaguzi. Hata hapa, nchini Marekani, tulishangazwa na kile kilichotokea Januari 6 kwenye jengo la Capitol. Kuna maendeleo mengi Afrika. Hivi sasa, kwa viongozi ambao wamekuwepo madarakani kwa muda mrefu, je utasema nini kama hiyo ndiyo nia ya watu? Chaguzi zina maana ya kuwauliza watu kutoa maoni yao. Je kama watu wanapiga kura wakipendelea uthabiti?

Baadhi ya nchi za kiafrika zimeona kutokea tena kwa mapinduzi, na katika kesiya Libya, mizozo sugu. Sassou-Nguesso alisema bila ya amani na usalama, maendeleo hayawezi kupatikana.

“Kama hatusuluhisho suala la Libya, hatutaona mwanga katika ukanda wa Sahel. Kwahiyo ugaidi na ghasia za msimamo mkali barani Afrika, tatizo linalohusiana na amani kwa jumla ni muhimu sana. Kama mwenyekkti wa kamati ya AU ya ngazi ya juu kwa Libya, tuko katika mchakato wakuandaa mkutano wa maridhiano.”

Libya imekuwa na amani kwa muda mfupi tangu mwaka 2011 kufuatia mapinduzi yaliyoungwa mkono na NATO ambayo yalimuondoa madarakani Moammar Gadhafi.

Sassou-Nguesso amekuwa ndani ya nje ya madaraka kwa kipindi cha miongo mitatu. Alipoulizwa kama atawania tena katika uchaguzi ujao, anasema kwa wakati huu anajaribu kutekeleza program ambazo zilimsaidia kuingia madarakani.

XS
SM
MD
LG