Hii ni kufuatia tukio la mafuriko yaliyoikumba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mji mkuu Kinshasa na kuua zaidi ya watu 120.
Katika ujumbe wa tweet, Bwana Tshisekedi anasema atarejea nyumbani Alhamisi baada ya mkutano wake na Rais Joe Biden.
Siku tatu za maombolezo zimetangazwa na rais ameziambia idara za serikali kuzisaidia familia zilizoathiriwa na kuanza kuijenga tena miundombinu.
Katika mkutano na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken Rais Tshisekedi alilaumu mafuriko hayo kwa kusema yamesababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa, shirika la habari la AFP limeripoti.