Kundi la wanamgambo linaloongozwa na watutsi walianzisha mashambulizi yao ya karibuni huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo mwezi Machi, na haraka kukamata miji kadhaa ya mashariki. Takriban watu 390,000 wamekoseshwa makazi kwasababu ya mapigano.
Ripoti ya awali ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa wiki iliyopita ilisemakuwa waasi wamewaua wana vijiji 131 katika vijiji vya Kishishe na Bambo na sehemu ya kampeni ya mauaji, ubakaji, utekaji nyara na wizi wa ngawira.
Hali nchini DRC inalingana na kile ambacho kinatokea nchini Ukraine kutokana na uvamizi wa Russia, Mukwege aliliambia shirika la habari la Reuters katika mahojiano yaliyofanyika Paris, Jumatatu.
Hatuwezi kwa upande mmoja kumshutumu au kukiri kwamba Rwanda imeishambulia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ikiwani ukiukaji wa sheria za kimataifa, ukiukaji wa mkataba wa Umoja wa Mataifa, na kwa upande mwingine, tuendelee kuisaidia kifedha Rwanda alisema.
Daktari Mukwege mtalaamu wa magonjwa ya kina mama na mwanaharakati ni mkurugenzi wa Hospitali ya Panzi Kivu Kusini, alishinda tuzo ya amani ya nobeli mwaka 2018 kwa juhudi zake za takriban miongo miwili kupambana dhidi ya manyanyaso ya ngono.