Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 20, 2024 Local time: 05:32

Kundi la waasi la M23 DRC lataka mazungumzo na serikali


Wanajeshi wa FARDC wakipambana na M23 Kivu Kaskazini Mashariki mwa Congo
Wanajeshi wa FARDC wakipambana na M23 Kivu Kaskazini Mashariki mwa Congo

Kundi la waasi wa M23 Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo Ijumaa limesema linataka kufanya mazungumzo na Serikali baada ya rais wa Congo na viongozi wengine wa Afrika kutia saini makubaliano ya kusitisha mapino na kuweka silaha chini yenye lengo ya kusitisha mashambulizi ya wanamgambo.

Viongozi wa Congo, Rwanda, Burundi, na Angola walikutana wiki hii huko Luanda kutafuta suluhu ya mzozo mashariki mwa Congo ambao umesababisha maelfu ya watu kukimbia nyumba zao.

Wametia saini wakisema kuwa wanasisitiza sitisho la mapigano kuanzia ijumaa, na kusema kuwa vikosi vya kieneo vitaingia dhidi ya kundi la M23 kama hawatajiondoa kutoka maeneo waliyokalia. Hata hivyo M23 haikuwa sehemu ya majadiliano hayo na iligundua kuhusu taarifa kwenye mitandao ya kijamii, msemaji wake amesema.

Serikali ya Congo imetupilia mbali kufanya mazungumzo na kundi la M23 mbalo inaliona kama la kigaidi. Alipoulizwa kuhusu hili katika Mkutano na waandishi wa habari Alhamisi, waziri wa mambo ya nje Christopher Lutundula alisema haiwezi kutokea. “ naweza kukuhakikisha kwa niaba ya serikali na Rais wa jamhuri ya Congo”

Hata hivyo M23 ilisema tayari ilitangaza kusitisha mapigano kwa upande mmoja mwezi April, na kwamba ni jeshi la Congo ambalo linaanzisha mashambulizi. Mapigano yameendelea tangu wakati huo, M23 imeteka miji kadhaa mashariki mwa Congo.

XS
SM
MD
LG