Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:18

Vita vya DRC vinasuluhishwa kidiplomasia au kijeshi?


Rais wa Kenya William Ruto (aliyekaa kushoto), Evariste Ndayishimiye wa Burundi (katikati) na rais mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta (kulia), pamoja na mjumbe maalum wa umoja wa mataifa katika mziwa makuu Huang Xia (wa 3 kutoka kulia kwa waliosimama) Nairobi Kenya Nov 28 ,2022
Rais wa Kenya William Ruto (aliyekaa kushoto), Evariste Ndayishimiye wa Burundi (katikati) na rais mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta (kulia), pamoja na mjumbe maalum wa umoja wa mataifa katika mziwa makuu Huang Xia (wa 3 kutoka kulia kwa waliosimama) Nairobi Kenya Nov 28 ,2022

Awamu ya tatu ya mazungumzo ya kutafuta amani mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imeanza katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi kwa kuzingatia namna yakutekeleza mpango wa kuleta mabadiliko yatakayopelekea makundi ya waasi kupokonywa silaha.

Rais wa Kenya William Ruto, na Evariste Ndayishimiye wamehudhuria kikao hicho huku marais wa Congo, Rwanda na Burundi wakihudhuria kwa njia ya video.

Viongozi hao wameeleza nia yao ya dhati kutaka usalama urejee mashariki mwa DRC.

Rais mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta, ambaye ndiye mjumbe maalum wa jumuiya ya Afrika mashariki kwa ajili ya DRC, amesema kwamba lengo kubwa ni kujadiliana kuhusu mchakato wa kisiasa na mabadiliko katika taasisi, yatakayoweka mazingira mema ya waasi kuweka chini silaha, kusaidiwa kuishi Maisha ya kawaida.

Viongozi waliohudhuria kikao cha wiki iliyopita nchini Angola, walikubaliana kuhakikisha kwamba mapigano yanasitishwa mara moja na waasi wa M23 kuondoka katika miji wanayoshikilia

Japo waasi wa M23 hawakuwepo rasmi kwenye kikao cha Angola, walisema kwamba hawataheshimu makubaliano hayo na kwamba hawana Imani kwamba serikali ya DRC itatekeleza mkataba huo na kuacha mashambulizi.

Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika mashariki Peter Mathuki amesema kwamba baadhi ya makundi ya waasi yamekuwa na waakilishi kwenye mkutano wa Nairobi, lakini hakutaja majina ya makundi hayo.

Mkakati wa kuzima vita vya DRC

Mjumbe wa jumuiya ya Afrika mashariki inapanga kutambua chanzo cha mgogoro wa DRC katika mikoa mitano na kuweka mikakati namna ya kurejesha utawala wa serikali katika mikoa hiyo ili amani ya kudumu ipatikane.

Hatua ya kutuma wanajeshi wa jumuiya ya Afrika mashariki nchini DRC pia itajadiliwa.

Wanajeshi wa Kenya tayari wameingia DRC. Jeshi la jumuiya ya Afrika mashariki litajumulisha pia vikosi kutoka Uganda, Burundi na Sudan kusini.

Kenyatta amesisitiza kwamba jumuiya ya Afrika mashariki inaweza tu kusaidia kurejesha amani nchini Congo lakini jukumu kubwa la kudumisha amani ni la watu wa Congo wenyewe.

Wapiganaji wa kundi la waasi la M23
Wapiganaji wa kundi la waasi la M23

Je, M23 wanapigania Watutsi au kusimamia utajiri wa madini?

Kundi la waasi la M23 lilipata umaarufu mwongo mmoja uliopita, lilipovamia na kudhibithi mji wa kibiashara wa Goma. Kundi hilo liliondoka baada ya kupatikana mkataba wa amani na baadhi ya wapiganaji wake kujiunga katika jeshi la serikali.

Kundi hilo lilianza tena vita Novemba mwaka uliopita, likidai kwamba serikali ya DRC imekosa kuheshimu ahadi zake. Lilidhibithi mji wa Bunagana, mpakani na Uganda mnamo mwezi June.

Kundi la M23 limekuwa likizungumziwa sana katika uhusiano unaoendelea kuharibika kati ya Congo na Rwanda. wengi wa apiganaji wa kundi hilo ni kutoka kabila la Watutsi. Rais wa Rwanda Paul Kagame pia anatoka kabila la Watutsi.

Lilipoanza vita, kundi la M23 lilidai kwamba lilikuwa linapigania maslahi ya Watutsi, lakini wachambuzi wanasema kwamba kundi hilo linapigania kudhibithi mashariki mwa DRC ili kuwa na uwezo wa kusimamia utajiri mkubwa wa madini ulio sehemuhiyo.

XS
SM
MD
LG