Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:34

Wakaazi mashariki mwa DRC wanaelezea hali ilivyo huko


Wakaazi huko mashariki mwa DRC wakikimbia nyumba zao kuepuka mapigano yanayoendelea huko
Wakaazi huko mashariki mwa DRC wakikimbia nyumba zao kuepuka mapigano yanayoendelea huko

Waasi wa M23 waliwaua raia wasiopungua 131 wakiwemo watoto 12 na walifanya ubakaji zaidi ya dazeni mbili hapo Novemba 29-30 katika vijiji viwili kwenye eneo la Rutshuru ikiwa ni pamoja na Kishishe, Umoja wa Mataifa unasema

Katika kambi ya wakimbizi Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC) Eric, Samuel, Tuyisenge na Florence walielezea yaliyowasibu walipotembea maili kadhaa wakikimbia shambulizi baya la waasi katika kijiji chao.

Waasi wa M23 waliwaua raia wasiopungua 131 wakiwemo watoto 12 na walifanya ubakaji zaidi ya dazeni mbili hapo Novemba 29-30 katika vijiji viwili kwenye eneo la Rutshuru, ikiwa ni pamoja na Kishishe, Umoja wa Mataifa unasema.

Kundi hilo limekanusha kuhusika, likilaumu "risasi zilizopigwa kiholela" kwa vifo vya raia wanane.

Lakini katika kambi ya Mungote, Eric Nesehose alisema hawezi kusahau alipowaona wapwa zake Jacques na Musayi wakipigwa risasi mbele ya macho yake.

"Walitoka nje ya nyumba, wakipiga kelele 'kuna milio ya risasi'," alisema.

"Risasi ziliwapiga wakiwa mlangoni na walifariki papo hapo."

Wakikimbia kuokoa maisha yao, Eric na wanavijiji wengine walitembea umbali wa kilomita 40 hadi 60 kuvuka milima hadi kambi ya Mungote wilayani Kitshanga.

Mashariki mwa DRC ilimekuwa eneo tete kwa miaka mingi, na ni makazi ya makundi yenye silaha.

Vuguvugu la M-23, ambalo ni kundi kubwa la Watutsi wa Kongo, lilianza tena mapigano mwishoni mwa mwaka 2021 baada ya kukaa kimya kwa miaka mingi.

Katika miezi ya karibuni kundi limechukua udhibiti wa sehemu kubwa katika eneo la Rutshuru kaskazini mwa mji wa Goma.

Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa (MONUSCO) kimesema hakikuweza kufika Kishishe na eneo jirani la Bambo kuchunguza mauaji ya mwezi uliopita, lakini walikusanya ushahidi kutoka kwa mashahidi na vyanzo vingine.

Wanasema ghasia dhidi ya raia zilikuwa za kulipiza kisasi kwa mapigano kati ya kundi la M23 na mengine, hasa makundi yenye silaha ya Kihutu.

XS
SM
MD
LG