Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:13

Idadi ya watu waliokufa kutokana na mafuriko DRC yafikia 140


watu wakiomboleza waliokufa kutokana na mafuriko DRC
watu wakiomboleza waliokufa kutokana na mafuriko DRC

Watu 140 wamethibitishwa kufariki na wengine kadhaa kujeruhiwa kafuatia mafuriko yaliyotokea sehemu mbalimbali katika mji mkuu wa Kinshasa, huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Waziri mkuu wa DRC Jean Michel Lukonde, amesema kwamba maafisa wanaendelea kutafuta miili zaidi ya watu wanaoaminika kufariki katika mafuriko hayo.

Karibu watu milioni 12 wanaishi katika mitaa iliyo karibu na mji wa Kinshasa, ambayo imekumbwa na mafuriko.

Nyumba kadhaa zimesombwa na maji na barabara kuharibiwa kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa.

Watu watano wa familia moja, akiwemo mtoto wa kike mwenye umri wa miaka tisa ni miongoni mwa waliofariki

XS
SM
MD
LG