Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:07

Wakimbizi wameandamana Rwanda kupinga mauaji ya raia mashariki mwa DRC


Raia wa DRC wanaoishi Rwanda kama wakimbizi wakiwa katika maandamano kupinga mauaji ya ndugu zao mashariki mwa DRC, December 13, 2022
Raia wa DRC wanaoishi Rwanda kama wakimbizi wakiwa katika maandamano kupinga mauaji ya ndugu zao mashariki mwa DRC, December 13, 2022

Wakimbizi kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wanaoishi nchini Rwanda, wamefanya maandamano kupiga mauaji yanayoendelea kutokea nchini mwao kila mara.

Maandamano yameanzia kwenye kambi ya wakimbizi ya Kigembe, wilaya ya Nyamagabe, kusini mwa Rwanda na kuenea hadi katika kambi ya Mahama iliyo mashariki mwa nchi hiyo karibu na Tanzania.

Maelfu ya wakimbizi hao wamebeba mabango yenye ujumbe unaokemea mauaji ya raia mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, ambapo makundi ya waasi yamekuwa yakitekeleza mashambulizi kila mara, kuua rai ana kusababisha uharibifu wa mali.

Wamekuwa wakiishi nchini Rwanda kwa karibu miaka 29. Wanataka jumuiya ya kimaifa kuingilia kati ana kuhakikisha kwamba amani inarejea DRC.

Bouna Lisale ni mkimbizi wa Jamhpuri ya Kidemokrasia ya Kongo na amaeshiriki maandamano hayo. Amesema kwamba alikimbilia Rwanda mwaka 2012 baada ya familia ya mume wake ambaye pia ni raia wa Congo mwenye asili ya Rwanda kushambuliwa, huku wakihusishwa na Rwanda.

Mapigano ya waasi mashariki mwa DRC

Kundi la waasi la M23 limekuwa likipigana na wanajeshi wa serikali mashariki mwa Jmahuri ya kidemokrasia ya Congo, vita ambavyo vimepelekea Rwanda na DRC kuingia katika mgogoro wa kidiplomasia.

DRC inadai kwamba waasi hao wanaungwa mkono na Rwanda, huku Rwanda ikidai kwamba serikali ndio sababu kubwa ya mgogoro huo kwa kuunga mkono waasi wa FDLR wanaohusishwa na mauaji ya kimbari nchini Rwanda.

Waasi wa M23 wamedai kwamba wanapigania haki za raia wa Congo wenye asili ya Kinyarwanda, wanaoishi mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Makundi mengine kama Allied democratic forces ADF, mai mai na Codeco, yamekuwa yakishambulia wakaazi mashariki mwa DRC na kusababisha vifo na idadi kubwa ya watu kukimbilia nchi Jirani kama wakimbizi, ikiwemo Rwanda na Uganda.

Imetayarishwa na Sylvanus Karemera, VOA, Kigali

XS
SM
MD
LG