Zimbambwe yakerwa na vikwazo vya Marekani dhidi ya balozi Sanyatwe

Hatua ya Marekani kumwekea vikwazo Anselem Nhamo Sanyatwe, balozi wake nchini Tanzania imeikera serikali ya Zimbabwe.

Vyanzo vya habari vinaeleza kuwa serikali ya Zimbabwe imeitaja hatua hiyo ya Marekani kama inayokadamiza uhuru wa taifa hilo.

Zimbabwe inasema hatua hiyo itapelekea mgawanyiko badala ya kuleta suluhisho la kitaifa'.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitangaza vikwazo dhidi ya Balozi Sanyatwe, ambaye ni Brigedia mstaafu ya jeshi la kitaifa la ulinzi wa rais, kutokana na "kuhusika kwake na ukiukaji wa haki za kibinadamu."

Anadaiwa aliongoza operesheni maalum ambayo ilitumia nguvu ya ziada kuwakandamiza waandamanaji wakati wakipinga matokeo ya uchaguzi Agosti mosi mwaka 2018 baada ya uchaguzi mkuu, uliyosababisha vifo vya raia sita

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imempiga marufuku ya kuingia Marekani Sayatwe aliyekuwa kiongozi wa kikosi maalum cha kijeshi cha kulinda Rais sasa anaelekea Tanzania akiwa balozi wa Zimbabwe nchini humo.

Chama kikuu cha upinzani cha Zimbabwe, makundi ya kutetea haki za binadamu pamoja na makundi ya kidini jana wameadhimisha mwaka mmoja tangu wanajeshi walipouwa darzeni ya waandamanaji waliokuwa wakilalamikia kucheleweshwa kwa matokeo ya uchaguzi uliofanyika mwezi Julai

Makundi yote yalioshiriki yalisema kuwa yataendelea kuomba Mungu aingilie kati taifa hilo la kusini mwa Afrika ambalo limekumbwa na ghasia kwenye mfumo wake wa kisiasa.

Wakati wa maadhimisho Alhamisi, chama kikuu cha upinzani kilisema kuwa lazima serikali iwafidie waliojeruhiwa kama Munesi pamoja na familia zilizopoteza watu wao.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.