Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:31

Upinzani Zimbabwe wakatisha hotuba ya Mnangagwa bungeni


[Speak Easy] 십년감수하다 'Close call'
[Speak Easy] 십년감수하다 'Close call'

Wabunge wa upinzani nchini Zimbabwe Jumanne walitoka nje ya bunge wakati wa hotuba ya kitaifa iliyokuwa inatolewa na Rais Emmerson Mnangagwa.

Wachambuzi wanailesa hatua hiyo kama ishara ya hasira ya wabunge hao baada ya kushindwa katika uchaguzi wa urais na bunge wa mwezi Julai mwaka huu.

Wanachama wa Movement for Democratic Change, MDC, wakiongozwa na kiongozi wao Nelson Chamisa, ambaye alishindwa na Mnangagwa kwenye uchaguzi huo, walianza kupiga kelele katika bunge, na baadaye kuondoka, muda mfupi baada ya Mnangagwa kuanza kusoma hotuba yake.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, baadaye wabunge hao walianza kuimba nyimbo za kukikashfu chama kinachotawala cha Zanu PF.

Kiongozi wa upinzani wa cahama cha upinzni cha Zimbabwe, MDC, Nelson Chamisa.
Kiongozi wa upinzani wa cahama cha upinzni cha Zimbabwe, MDC, Nelson Chamisa.

Lakini kwenye hotuba yake, Mnangagwa alisisitiza kwamba suala la uchaguzi wa mwezi Julai ni historia, na kwamba sasa ni wakati wa wanasiasa kutekeleza ahadi walizozitoa kwa wapiga kura.

XS
SM
MD
LG