FAO: Takriban tani milioni 25 za nafaka zimekwama Ukraine

FILE PHOTO: Dereva akishusha nafaka kwenye ghala msimu wa mavuno huko katika kijiji cha Zhovtneve, Ukraine, Julai 14, 2016 REUTERS/Valentyn Ogirenko/File Photo

Takriban tani milioni 25 za nafaka zimekwama nchini Ukraine na haziwezi kuondoka nchini humo kutokana na changamoto za miundombinu na kuzuiwa kwa bandari za black sea ikiwemo Mariupol afisa wa shirika la chakula la Umoja wa Mataifa amesema Ijumaa.

Kuzuiwa huko kunaonekana ni kama sababu ya ongezeko la bei ya chakula ambayo imevunja rekodi mwezi March kufuatia uvamizi wa Russia nchini Ukraine, kabla ya kupungua nguvu mwezi April , FAO imesema ijumaa.

Ukraine ilikuwa nchi ya nne kwa uuzaji mahindi nje ya nchi duniani, katika kipindi cha mwaka 2020 na 2021 na ni namba sita kwa uuzaji nje wa ngano, hiyo ni kwa mujibu wa data za baraza la kimataifa la nafaka.

Tangu Moscow ilipoanzisha kile ilichokiita operesheni maalumu za kijeshi mwezi Februari, Ukraine imelazimika kununua nafaka nje kwa njia ya treni kupitia mpaka wake wa magharibi au bandari zake ndogo kwenye ziwa Danube mahali ilipo bandari.