Raia wamekabiliwa na unyanyasaji kama vile kufyatuliwa risasi na mateso kutoka kwa wanajeshi wa Russia mapema wakati Russia ilipofanya uvamizi, kundi hilo la kutetea haki za binadamu limesema katika taarifa yake iliyochapishwa Ijumaa.
Katibu Mkuu wa Amnesty Internatinal Agnes Callamard ameeleza: “Ushahidi tuliokusanya tangu uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine ulipoanza mwishoni mwa mwezi February mwaka 2022, umeonyesha jeshi la Russia lilikiuka sheria za kimataifa, ikiwemo mauaji kiholela, mashambulizi yasiyo ya lazima na ya kibaguzi dhidi ya raia, ikiwa ni pamoja na kwenye makazi yenye watu wengi. Usambazaji wa mabomu ambao yamepigwa marufuku ikiwa ni kinyume cha sheria za kimataifa .”
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Agnes Callamard: “Unyanyasaji dhidi ya raia waliozingirwa na kushindwa kulinda njia za kibinadamu. Kwa maeneo mengine, tunajua kwamba uhalifu uliofanyika dhidi ya watu wanaoishi kuzunguka Kyiv, ambayo tunaripoti leo sio hadithi tu, bahati nasibu, au dhamana. Tunajua wao ni sehemu ya muundo wa tabia ya Russia ya uhasama tangu mwanzo. Tukio linalojirudia la kiwango cha juu lenye matokeo mabaya.”
Ripoti hiyo imehitimisha kwamba wanajeshi wa Russia wamefanya uhalifu wa vita huko Bucha, ikiwemo mauaji kinyume cha sheria. Mengi yakiwa karibu na makutano ya mitaa ya Yablunska na Vodoprovidna.
Uchunguzi wa shirika la habari la ROITA uliochapishwa Alhamisi umejumuisha ushuhuda, na ushahidi uliolenga mitaa wa Yablunska kwa utambulisho wa wanajeshi binafsi wa Russia na vitengo vya kijeshi vilivyopo Bucha.