Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 28, 2024 Local time: 16:45

Human Rights Watch inasema wanajeshi wa Russia waliua raia nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati


Mlinzi wa kibinasfi kutoka kundi la Russia , Wagner akisimama karibu na mwanajeshi wa Jamuhuri ya Afrika ya kati kwenye mkutano wa chama tawala cha MCU mjini Bangui, March 18, 2022. Picha ya AFP
Mlinzi wa kibinasfi kutoka kundi la Russia , Wagner akisimama karibu na mwanajeshi wa Jamuhuri ya Afrika ya kati kwenye mkutano wa chama tawala cha MCU mjini Bangui, March 18, 2022. Picha ya AFP

Shirika linalotetea haki za binadamu Human Rights Watch Jumanne limesema kuna ushahidi wa kutosha kwamba wanajeshi wa Russia wamefanya vitendo vibaya vya ukiukwaji wa haki za binadamu na kuua raia nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati mwaka wa 2013 kati ya makundi mengi ya wanamgambo na serikali yenye udhaifu mkubwa, vilipungua sana katika miaka ya hivi karibuni.

Lakini mwaka mmoja uliopita, mapigano yalizuka tena wakati waasi walipoanzisha mashambulizi ya kutaka kumuondoa madarakani Rais Faustin Archange Touadera.

Baada ya rais kuiomba msaada Moscow, mamia ya wanajeshi wa Russia waliisaidia serikali kuwarudisha nyuma waasi, ambao walikuwa bado wanadhibiti baadhi ya maeneo ya nchi.

Wanajeshi hao wakandarasi wa kibinafsi wanaelezewa mara nyingi kuwa ni kutoka kundi la Wagner, kampuni ya Russia ambayo hadhi yake ya kisheria haijulikani.

“Vikosi nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati, ambavyo mashahidi walivitambulisha kuwa Warussia, inasemekana vilua kiholela, kutesa na kupiga raia tangu mwaka wa 2019,” Human Rights Watch imesema.

“Serikali kadhaa za magharibi, wataalamu wa Umoja wa mataifa na wachunguzi maalum walipata ushahidi kwamba vikosi vyenye uhusiano na Russia vinavyofanya kazi nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati vinajumuisha idadi kubwa ya wafanyakazi wa kundi la Wagner, mkandarasi wa kibinasfi wa Russia wa masuala ya kijeshi na kiusalama ambalo lina uhusiano na serikali ya Russia,” Human Rights Watch imeongeza.

XS
SM
MD
LG