Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 28, 2024 Local time: 00:33

Spika Pelosi afanya ziara ya kushtukiza Ukraine


Spika wa Baraza la wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi na Rais wa Ukraine President Zelenskiy walipokutana mjini Kyiv Jumamosi Aprili 30, 2022.
Spika wa Baraza la wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi na Rais wa Ukraine President Zelenskiy walipokutana mjini Kyiv Jumamosi Aprili 30, 2022.

Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, Nancy Pelosi, na wabunge wanne wa chama cha Democratic wametembelea mji wa Kyiv, Ukraine, na kukutana na Rais wa nchi hiyo Volodymyr Zelenskyy.

Pelosi amewambia Zelenskyy kwamba ziara hiyo ilikusudiwa kutoa shukrani na kuipongeza Ukraine kwa kupigania uhuru wake, na kwamba dhamira ya Marekani ni kuiunga mkono nchi hiyo hadi mapambano hayo yatakapomalizika.

Walioandamana na Pelosi walikuwa Wawakilishi Adam Schiff wa California, Jim McGovern wa Massachusetts, Gregory Meeks wa New York na Jason Crow wa Colorado.

Shambulio la kombora la Russia kwenye uwanja wa ndege wa Odesa siku ya Jumamosi liliharibu kabisa barabara ya ndege, kiasi cha kutoweza kupitika, jeshi la Ukraine liliripoti.

Shahidi mmoja aliiambia CNN kwamba aliona angalau ndege moja ya kivita kwenye mji huo wa kusini mwa Ukraine, na kwamba milipuko hiyo ilisikika mara baada ya ving'ora vya mashambulizi ya anga kusikika katika jiji lote.

Vikosi vya Russia pia vilishambulia eneo la Donbas mashariki mwa Ukraine Jumamosi, lakini vilishindwa kutwaa maeneo matatu yaliyolengwa, jeshi la Ukraine lilisema. Kwingineko, polisi wa Ukraine walisema wamepata miili ya watu watatu raia wa kawaida katika wilaya ya Bucha, kaskazini mwa Kyiv. Polisi walisema miili hiyo ilikuwa kwenye shimo na mikono ya waathiriwa ilikuwa imefungwa, macho yao yalikuwa yamefunikwa na wawili walikuwa wamezibwa mdomo.

Kyiv anasema zaidi ya miili 1,000 imegunduliwa ndani au karibu na Bucha. Gavana wa eneo la Kursk magharibi mwa Russia alisema makombora kadhaa yalirushwa Jumamosi kwenye kituo cha ukaguzi karibu na mpaka wake kutoka upande wa Ukraine.

XS
SM
MD
LG