Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:05

Pelosi achaguliwa tena spika wa bunge la Marekani


Nancy Pelosi akiinua rungu la spika baada ya kuchaguliwa tena kuwa spika wa bunge la Marekani
Nancy Pelosi akiinua rungu la spika baada ya kuchaguliwa tena kuwa spika wa bunge la Marekani

Mwakilishi Nancy Pelosi alichaguliwa tena kuwa spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Jumapili kwa kipindi chake cha nne, akiwa na wingi uliopungua wa wawakilishi wa chama cha demokrat na changamoto zilizo mbele.

Mdemokrat huyo kutoka jimbo la California alipata kura zilizohitajika kupata ushindi Jumapili alasiri, na huku Wademokrat wawili wakipigia kura wagombea wengine na wengine watatu wakipiga kura ya kusema walikuwapo.(bila kuunga mkono wala kukataa).

Wademokrat wanashikilia wingi wa baraza la wawakilishi kwa idadi ndogo katika Baraza jipya la 117, wakiwamo wademokrat 222 na Warepublican wapatao 211. Wawakilishi wengine wachache hawakuweza kupiga kura kwa sababu walikuwa wameambukizwa virusi vya korona au walikuwa na shida zingine za kiafya.

Kwa mara ya kwanza tangu Mei, wabunge walipaswa kuwapo kwenye upigaji kura kura badala ya kutumia mfumo wa mtandao uliowekwa katikati ya janga hili. Kura hiyo ilidumu kwa saa kadhaa wakati wabunge waliletwa ndani ya ukumbi katika vikundi vidogo vidogo ili kuepusha idadi kubwa ya wajumbe katika ukumbi.

Bunge jipya linakabiliwa na changamoto kadhaa, kati yake kulishinda janga la corona ambalo hadi sasa limegharimu maisha ya wamarekani zaidi ya 350,000, na kufufua uchumi wa nchi.

Pelosi mwenye umri wa miaka 80 ameonyesha kuwa baada ya kipindi hiki cha miaka miwili hatagombea muhula mwingine kama spika wa Bunge, kulingana na makubaliano yaliyofanywa na Wanademokrat mnamo mwaka 2018 ambapo walimtaka asigombee uspika wakati huo.

Imetayarishwa na Sunday Shomari VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG