Kuondolewa kwa wanaume 41 wafanyakazi wa kima cha chini kutoka kwenye baadhi ya majimbo masikini sana nchini India, kulianza zaidi ya saa sita baada ya waokoaji kuvunja katika vifusi kuelekea kwenye handaki hilo katika jimbo la Uttarakhand ambako walikwama tangu Novemba 12.
“ Tulikuwa 41 na wote kutoka majimbo tofauti, wote tulikuwa kama kaka , “ alisema hayo Saba Ahmed mmoja wa wafanyakazi 41 waliookolewa.
Wafanyakazi hao pia walimwambia Modi walikuwa wanatembea huko chini ya ardhi na kufanya mazoezi ya Yoga nyakati za asubuhi ambayo yaliwasaidia kuwa vizuri.
Wafanyakazi hao hivi sasa wako katika hospitali na wanatarajiwa kwenda kwenye majimbo yao baada ya madaktari kuwaruhusu.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.