Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 05, 2025 Local time: 06:04

India yafuatilia wanajeshi wake waliohukumiwa kifo Qatar


Waziri wa mambo ya nje wa India
Waziri wa mambo ya nje wa India

Waziri wa mambo ya nje wa India amesema nchi hiyo itafanya juhudi zote kuhakikisha kuachiliwa huru kwa wanajeshi wanane wa zamani wa jeshi la majini waliohukumiwa kifo na mahakama nchini Qatar, wakiripotiwa kufanya ujasusi kwa Israel.

Subrahmanyam Jaishankar alisema alikutana na familia za raia hao wa India waliokamatwa na kuwaambia serikali “inaiangalia kwa makini” kesi yao.

Vyombo vya habari vya India vinaripoti kuwa maafisa hao wanane, miongoni mwao maafisa wa zamani wa ngazi ya juu, wakiwemo manahodha ambao wakati mmoja walikuwa wanaendesha meli za kivita, walikamatwa mjini Doha mwezi Agosti 2022.

Katika ujumbe kwenye mitandao ya kijamii, Jaishankar alisema kuwa ameelezea kikamilifu “wasiwasi na uchungu walio nao familia”, na kwamba “serikali itaendelea kufanya juhudi zote za kuhakikisha kuachiliwa kwao”.

Forum

XS
SM
MD
LG