Wizara ya ulinzi ya Uturuki imetangaza kuwasili kwa sehemu ya kwanza ya shehena ya mfumo wa silaha za ulinzi wa anga aina ya S-400, kutoka Russia.
Ndege ya mizigo ya Russia, iliwasili ikiwa imebeba shehena ya mfumo wa silaha hizo katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Murted, Ankara.
Silaha hizo kutoka Russia, za kwanza kuuzwa kwa mwanachama wa Umoja wa Kujihami wa Ulaya, Nato, imesababisha wasiwasi kwamba Uturuki inakaribia ushawishi wa Moscow.
Uturuki ilikuwa imekataa kuzingatia masharti ya Marekani kujiondoa kwenye mkataba huo, ulioripotiwa kugharimu zaidi ya dola bilioni 2.
Imetayarishwa na mwandishi wetu Washington, DC