Ushindani mkali California huenda ukaamua nani atadhibiti Baraza la Wawakilishi

FILE PHOTO: Rais wa Marekani Joe Biden

Ni mapema mno - kutangaza mshindi wa uchaguzi wa California hii inaendelea kusikika na huenda itamalizika kwa kuamua iwapo Warepublikan watadhibiti Baraza la Wawakilishi au Wademokratik wataendelea kushikilia madaraka.

Huku mamilioni ya kura zikiwa hazijahesabiwa hadi Jumatano kote katika jimbo la Marekani lenye idadi kubwa zaidi ya watu, haijulikani hatma ya takriban darzeni ya wagombea 52 wa Baraza la Wawakilishi katika jimbo hilo.

FILE -Katie Porter

Huko kusini mwa California, Wawakilishi Wademokratik Katie Porter na Mike Levin wamebanwa na ushindani mkali, licha ya Rais Joe Biden kufanya kampeni saa ya mwisho kwa niaba yao.

Mashariki ya Los Angeles, Mwakilishi Mrepublikan Ken Calvert alikuwa nyuma ya Mdemokrat Will Rollins kwa pointi 12, lakini chini ya thuluthi ya kura zilizokuwa zinatarajiwa zimeshajumlishwa.

FILE - David Valadao,

Huko Central Valley, Mwakilishi wa chama cha Republikan David Valadao, ambaye alipiga kura kumuondoa madarakani Rais Donald Trump, asilimia 54 ya kura zilizohesabiwa hadi sasa katika kinyang’anyiro hicho dhidi ya Mdemokrat Rudy Salas, lakini kura nyingi bado hazijajumlishwa.

Miaka minne iliyopita, Valadao alishindwa katika kugombea tena baada ya kushuhudia ushindi wa kiasi Siku ya Uchaguzi ukitoweka pale kura zilizochelewa kuwasili kwa njia ya posta kuhesabiwa. Lakini alishinda tena kiti chake mwaka 2020.

Endapo Wademokrat watashinda Calvert na kuongoza katika chaguzi nyingine ambako wanaongoza au watakuwa nyuma kidogo, mwaka huu utakuwa na kumbukumbu za mwaka 2018, wakati chama hicho kiliposhinda viti saba vilivyokuwa vikishikiliwa na Warepublikan wakielekea kulichukua baraza la Wawakilishi.

Lakini iwapo Calvert itabakia ilivyo na Warepublikan wakimtoa Porter na Levin na kushinda kiti kilichowazi katika eneo la Central California, hali itafanana na ile ya 2020, wakati wagombea wa chama cha Republikan katika Baraza la Wawakilishi waliposhinda viti vinne katika jimbo ambapo wademokrat waliosajiliwa wanawazidi Warepublikan kwa idadi ya 2-1.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP