Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 16:06

Matokeo ya uchaguzi Marekani yaendelea kutangazwa


Maafisa wa uchaguzi Marekani.
Maafisa wa uchaguzi Marekani.

Wamarekani wanaendelea kupokea na wengine kusubiri matokeo ya uchaguzi wa katikati ya muhula uliofanyika Jumanne.

Wapigaji kura uliendelea kwa utulilivu katika sehemu nyingi za nchi, huku viti vyote 435 vya baraza la wawakilishi na zaidi ya teheluthi moja ya vile vya seneti, pamoja na vingine vya magavana, vikishindaniwa.

Hadi tukitayarisha ripoti hii, vyombe kadhaa vya habri vilikuwa vimetangaza kwamba kiti cha gavana wa Florida kilikuwa kimechukuliwa na Mrepublika huku jimbo la Maryland likimchagua Mdemokrat.

Ushindani ulikuwa mkali kwa kiti cha seneti cha jimbo la Georgia.

Awali, matatizo ya kiufundi katika mashine za kupigia kura na kura yalishuhudiwa katika baadhi ya vituo jana Jumanne na kuwafanya maafisa wa uchaguzi kuhangaika huku wakiwahakikishia wapiga kura juu ya uadilifu wa uchaguzi wa Marekani, baada ya miaka miwili ya madai yasiyo na msingi ya udanganyifu, yaliyoathiri imani ya baadhi ya watu katika mfumo wa demokrasia.

Changamoto ziliripotiwa katika jimbo la Georgia, ambako mashindanio makali kwenye kitii cha seneti yalitarajiwa, na misururu mirefu ilionekana huko Texas baada ya baadhi ya mashine kuharibika.

Wakati huo huo, baadhi ya mashine za kupigia kura katika sehemu moja ya Arizona hazikuwa zikifanya kazi, katika kaunti ambayo ilishuhudia vuta ni nikuvute kubwa ya kisiasa katika uchaguzi mkuu uliopita ambako baadhi ya wafuasi wa raia wa zamani wa Marekani Donald Trump, wamekuwa wakidai kwamba uchaguzi huo wa mwaka 2020 uligubikwa na wizi.

Maafisa katika Kaunti ya Maricopa, ambayo inajumuisha Phoenix, jiji la tano lenye wakazi wengi nchini Marekani, walisema idadi ndogo ya vituo 223 vya kupigia kura vinakabiliwa na matatizo.

XS
SM
MD
LG