Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 15:44

Marekani: Kura zinaendelea kuhesabiwa

Wafanyakazi wa uchaguzi wanaendelea kuhesabu kura za uchaguzi wa katikati ya muhula nchini huko Georgia nchini Marekani.
Wafanyakazi wa uchaguzi wanaendelea kuhesabu kura za uchaguzi wa katikati ya muhula nchini huko Georgia nchini Marekani.

Udhibiti  wa Baraza la Seneti na Baraza la Wawakilishi nchini Marekani bado haujakamilika muda huu, wakati kura zikiendelea kuhesabiwa kutoka uchaguzi wa katikati ya muhula. Hii ni habari inaendelea kujitokeza na tutawajulisha kila mara leo Jumatano Novemba 9.

Hadi Jumatano asubuhi, kura katika majimbo mengi bado hazijajumlishwa na matokeo ya mwisho kutangazwa.

Wafanyakazi wa uchaguzi wakiweka kura zilizopigwa kwa njia ya posta katika mashine ya kuhesabu kura wakati wa uchaguzi wa katikati ya muhula huko Huntington Place, Detroit, Michigan, Marekani Novemba 8, 2022. REUTERS/Rebecca Cook

Lakini kwa kifupi hadi sasa wachambuzi wametabiri kile kilichoitwa “Wimbi Jekundu” la ushindi mkubwa wa Republikan halikutokea katika Senate, na viti walivyoongeza katika chama chao ndani ya Baraza la Wawakilishi huenda vinaweza kuwapa udhibiti, lakini siyo kwa ziada kubwa ya viti vya Warepulikan.

Kuna uwezekano wa Chama cha Demokratik kuendelea kudhibiti Baraza la Seneti – na hata upo uwezekano wa kupata kiti kimoja au viwili ili kukifanya kuwa na “wingi” kuliko ilivyokuwa hivi sasa “kuwa sare” kukiwa na Maseneta Warepublikan 50, na Wademokrat 48 na wawili huru ambao hupiga kura na chama hicho, huku Makamu wa Rais Kamala Harris akiwa ameshikilia “kura ya maamuzi” kwa ajili ya Wademokrat.

XS
SM
MD
LG