Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:02

Uchaguzi wa kati kati ya mhula Marekani unafanyika leo


Jengo la bunge la Marekani NOV 7. 2022
Jengo la bunge la Marekani NOV 7. 2022

Wapiga kura nchini Marekani wanapiga kura hii leo katika uchaguzi wa katikati ya muhula ambao matokeo yake yataamua iwapo chama cha Democrat kitaendelea kudhibiti baraza la wwawakilishi na senate.

Matokeo ya uchaguzi huu yana umuhimu mkubwa kwa utawala wa rais Joe Biden katika kutekeleza ajenda za serikali kuu katika muda wa miaka miwili ijayo.

Kulingana na historia ya siasa za Marekani, chama kilicho madarakani huwa kinashindwa katika uchaguzi wa katikati ya mhula na ukusanyaji wa maoni unaonyesha kwamba chama cha Republican kitashinda uchaguzi wa leo.

Mfumko wa bei, kuongezeka kwa uhalifu ndizo hoja kuu za chama cha Republican katika uchaguzi huu huku chama cha Democrat kikiangazia zaidi haki ya wanawake kutoa mimba na uvamizi uliofanywa na wafuasi wa aliyekuwa rais Donald Trump kuvamia majengo ya bunge Januari 6, 2021

Viti 35 vya senate na 435 vya baraza la Congress vinagombaniwa hii leo. Warepublican wanahitaji viti 5 kudhibithi senate.

Ushindani mkali unatarajiwa katika majimbo ya Pennsylvania, Nevada, Georgia na Arizona.

XS
SM
MD
LG