Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 18:22

Habari feki zasambazwa kwa wafuasi wa Trump, zikieneza uvumi wa kura kuibiwa


Election 2024 Trump
Election 2024 Trump

Maafisa wa uchaguzi kote Marekani wamejikuta wako katika dimbwi la mvutano Jumanne, wakijaribu kuzima juhudi za ndani ya nchi na za baadhi ya wanachama wakereketwa kuchukua dosari zilizosambaa za upigaji kura na kuzitumia kama ushahidi wa kuhujumu kwa kiasi kikubwa uchaguzi wa katikati ya muhula.

Tahadhari kuhusu uwezekano wa uchaguzi kuchakachuliwa zimekuwa zikisambaa kwa wiki kadhaa katika tovuti na mitandao mbalimbali ya kijamii inayopendelewa na wanasiasa waconservative na wanaomuunga mkono Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, wengi wao wanaendelea kuamini kuwa uchaguzi wa rais wa Marekani 2020 uliibiwa licha ya kutokuwepo ushahidi.

Madai hayo yamepata tena uhai mpya mapema Jumanne baada ya maafisa wa New Jersey na huko Arizona kuripoti vifaa vya eletroniki vya kukagua karatasi za kupiga kura vilikuwa na matatizo.

“Tunajaribu kutatua hili tatizo,” Kaunti ya Maricopa, Arizona, Mwenyekiti wa Bodi ya Wasimamizi Bill Gates alisema katika ujumbe wa video uliobandikwa katika mitandao ya kijamii, akiongeza kuwa hata hivyo tatizo hilo limeathiri asilimia 20 ya maeneo ya kupiga kura katika kaunti hiyo, na hatua mbadala zilizopo zitahakikisha kura zote zitahesabiwa.

Licha ya juhudi ya Gates na maafisa wengine wa Kaunti ya Maricopa kuwasiliana na wapiga kura, madai ya kuwepo makosa yalienea kwa haraka.

“Watu wanatakiwa kukamatwa kwa kile kinachotokea huko Kaunti ya Maricopa. Ni uhalifu,” alituma ujumbe wa tweet Charlie Kirk, muasisi wa taasisi ya harakati ya vijana waconservative Turning Point USA.

Wapiga kura wakisubiri katika mistari kupiga kura wakati wa uchaguzi wa katikati ya muhula huko Kaunti ya Maricopa mjin Cave Creek, Arizona Nov. 8, 2022.REUTERS/Brian Snyder
Wapiga kura wakisubiri katika mistari kupiga kura wakati wa uchaguzi wa katikati ya muhula huko Kaunti ya Maricopa mjin Cave Creek, Arizona Nov. 8, 2022.REUTERS/Brian Snyder

Muungano wa watafiti, Election Integrity Partnership, ulijikita katika kuhakikisha usalama wa uchaguzi, umesema umetambua kulitumwa zaidi ya tweets 40,000 kuhusu matatizo kadhaa huko Arizona katika kipindi cha muda wa saa mbili tangu mwanzo wa kuripotiwa mashine kuharibika.

Picha za video zikionyesha mistari mirefu huko katika Kaunti Maricopa na za maafisa wa uchaguzi pia zilijitokeza mitandaoni, baadhi zikionyesha wapiga kura wakieleza wamechukizwa na wafanyakazi wa uchaguzi wakati wakijaribu kuwaelezea sababu za uchelewesho huo.

Katika muda wa saa kadhaa, Trump yeye mwenyewe alikuwa anachangia katika lawama zilizokuwa zinaongezeka.

“Kuna vitu vingi vibaya vinaendelea,” rais wa zamani alisema kuhusu Kaunti ya Maricopa katika video iliyobandikwa katika mitandao ya kijamii ya kikundi cha Truth Social.

“Wanataka kuwachelewesha ili msiweze kupiga kura. … Sio haki kabisa hiki kinachofanyika.

Katika ujumbe mwingine, Trump aliwasihi a wafuasi wake “andamaneni, andamaneni, andamaneni!” baada ya kudai kuliko na matatizo yaliyosambaa huko Detroit, Michigan.

XS
SM
MD
LG