Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:03

Wamarekani milioni 35 wapiga kura kabla ya siku ya uchaguzi


US Election Arlington
US Election Arlington

Zaidi ya Wamarekani milioni 35 tayari wamepiga kura katika zoezi la uchaguzi wa nusu muhula linalondelea kote nchini, huku Warepublikan wakitabiri Jumapili kwamba watachukua udhibiti wa mabaraza yote mawili ya bunge kutoka kwa Wademokrat.

Haya yamefanyika zikikiwa zimesalia siku moja tu kabla ya uchaguzi muhimu wa nusu muhula kubaini ni mrengo upi utakaopata viti vingi katika nusu ya pili ya muhula wa miaka minne, wa Rais wa mrengo wa Demokratic Joe Biden.

Mradi uitwao Election in America umesema idadi ya wapiaga kura wa mapema imepita ile wakati wa chaguzi za miaka ya 2014 na 2018, ambazo zilifanyika katikati ya mihula ya marais Barack Obama na Donald Trump.

Sheria za upigaji kura zilibadilishwa katika majimbo mengi kabla ya uchaguzi wa rais wa 2020, wakati Biden alimshinda Trump, ili kurahisisha njia ya upigaji kura wa mapema, ili kuondoa hofu ya wapiga kura wengi.

Sasa, wapiga kura wengi wamezoea kupiga kura kabla ya Siku ya Uchaguzi, haswa wanachama wa chama cha Demokratik.

Wakati huo huo, Trump, akiashiria mara kwa mara kwamba anakaribia kutangaza kampeni ya urais 2024, na baadhi ya Warepublican wengine mara kwa mara wakikosoa upigaji kura wa mapema, wanadai bila ushahidi, kwamba unaongeza udanganyifu.

Viti vyote 435 katika Baraza la Wawakilishi na viti 35 kati ya 100 vya Seneti vinagombaniwa.

Wanademokrasia wameshikilia udhibiti mdogo zaidi katika mabunge yote mawili tangu mapema 2021, hali ambayo imemuwezesha Rais Biden kuendeleza baadhi ya vipaumbele vyake vya sera, lakini mara nyingi akikabiliwa na upinzani kutoka kwa Warepublican.

XS
SM
MD
LG