Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 04:21

Nitatangaza hivi karibuni kama nitagombea urais mwaka 2024 - Biden


Rais wa Marekani Joe Biden.
Rais wa Marekani Joe Biden.

Rais Joe Biden alisema Jumatano kuwa atatangaza mapema mwaka ujao iwapo atagombea tena urais. Alikuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari huko ikulu mjini Washington DC katika siku ambayo Wademokrat walikuwa wakielezea kuridhika kwao na matokeo ya uchaguzi wa katikati ya muhula.

Biden, mwenye umri wa miaka 79, na ambaye amekuwa mstari wa mbele kuwarai wapiga kura kuwachagua wanasiasa wa chama cha Demokratik, alielezea furaha yake baada ya matokeo kuashiria kwamba huenda chama cha Republikan kisipate viti vingi kwenye mabaraza yote mawili ya bunge, kama ilivyotabiriwa na wachambuzi.

"Tumefanya vizuri, Na huu ni mwanzo tu" alisema Biden.

Waandishi wawili walitaka kujua kama atagombea muhula wa pili, na kama atafanya hivyo, ni lini atatangaza azma yake.

"Nafikiri kila mtu anataka nigombee urais, lakini tutajadiliana kuhusu suala hilo. Sioni haja ya kuharakisha uamuzi huo, kwa njia moja au nyingine, iwe ni kesho, kesho kutwa au wakati mwingine wowote. Nadhani itakuwa mapema mwaka ujao ambapo nitafanya uamuzi huo," alisema Rais Biden

Udhibiti wa Baraza la Seneti la Marekani haukuwa umebainika wazi Jumatano usiku huku Warepublican wakikaribia kupata wabunge wengi wa baraza la wawakilishi, siku moja baada ya Wademokrat kuvuka matarajio ya wengi katika uchaguzi wa katikati ya muhula wa Marekani.

Matokeo ya mashindano ya kuwania viti vya Seneti katika majimbo ya Nevada na Arizona, ambako viongozi walioko madarakani wa chama cha Demokratik walikuwa wakimenyana na wapinzani wa Republikan, bado hayajatangazwa rasmi, huku maelfu ya kura zikiwa bado hazijahesabiwa.

Iwapo vyama hivyo vitagawanya viti hivyo, basi hatima ya Seneti itaangukia katika uchaguzi wa marudio wa Georgia kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka miwili, baada ya Edison Research kukadiria kuwa si mwaniaji aliyemaliza muda wake wa chama cha Demokratik Raphael Warnock wala Herschel Walker wa Republikan ambaye angefikia asili mia 50 ya kura zinazohitajika ili kuepusha uchaguzi wa marudio hapo Desemba 6 mwaka huu.

Wanachama wa Republikan walichukua angalau viti 10 katika Baraza la Wawakilishi la Marekani, utafiti wa Edison unakadiria. Hivyo vitakuwa viti tatu zaidi ya vinavyonahitajika ili kunyakua udhibiti kutoka kwa wademokrat.

XS
SM
MD
LG