Siku ya Jumamosi, maafisa hao walikamata kikundi cha wahamiaji haramu 37 kutoka Afrika ya Kati ambao walikuwa wamevuka mpaka eneo la Rio Grande wakiingia katika ardhi ya Marekani, CBP imesema katika taarifa yake Jumanne.
Ofisi hiyo imesema katika kundi hilo la wahamiaji kulikuwa na makundi ya wanafamilia, wakiwemo watoto wadogo, kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Jamhuri ya Congo.
Alhamisi iliyopita jioni, maafisa wa uhamiaji walikikamata kikundi cha wahamiaji kutoka Afrika cha watu 116 wakivuka mto kuingia eneo la Del Rio, CBP imesema katika taarifa yake ya Mei 31, 2019.
Kundi hili ni la kwanza kwa ukubwa kukamatwa katika eneo la Del Rio, ofisi hiyo CBP imesema. Eneo la mpaka wa Del Rio –Acuna liko takriban kilomita 260 (maili 160) ya mji wa San Antonio ulioko magharibi yaTexas.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.