Ugiriki inatarajiwa kuwasilisha pendekezo katika mkutano wa viongozi wa kitaifa huko Uhispania wiki hii lakini kufikia makubaliano kati ya wanachama 27 wa EU inaweza kuwa ngumu.
Waziri wa uhamiaji wa Ugiriki Dimitris Keridis alibainisha pendekezo hilo wakati serikali mjini Athens ikiwa inazidi “kupata wasiwasi na kuchukua tahadhari,” kama alivyoeleza, kuhusu mgogoro mpya wa uhamiaji.
Wasiwasi umeongezeka wakati idadi ya wahamiaji haramu wanaowasili Ugiriki ikiongezeka kufikia 31,000 mwaka huu, ikiwa imepanda kutoka 18,000 kwa mwaka mzima wa 2022.
Hali hii imetokea takriban muongo moja baada ya taifa maskini sana Ulaya kushuhudia zaidi ya wahamiaji milioni moja, wengi kutoka Syria, wakimkbizi wakiwasili katika mipaka yake na katika miji mikuu ya Ulaya, katika wimbi kubwa zaidi la uhamiaji kuwasili Magharibi tangu Vita vya Pili vya Dunia.
Wakati takriban wahamiaji 680,000 wamehalilishwa tangu mwaka 2021, Keridis alisema kiasi cha wahamiaji 60,000 bado wanaishi nchini kinyume cha sheria.
Alisema idadi yao inaendelea kuongezeka kwa sababu nchi kama vile Pakistan na Iran zinakataa kuwapokea raia wake ambao wanarejeshwa makwao kwa nguvu.
Alisema kuwa EU kwa ujumla itatakiwa kuzishinikiza nchi hizi kuwachukua wahamiaji wao haramu, au watakabiliwa na vikwazo.
Ripoti ya mwandishi wa VOA Anthee Carassava.