Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von de Leyen na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni walizuru kituo cha wahamiaji Jumapili kwenye kisiwa kidogo cha Lampedusa nchini Italia.
Kituo hicho hivi karibuni kilizidiwa na wahamiaji karibu 7,000 katika kipindi cha saa 24, jumla ambayo ni karibu sawa na idadi ya watu wanaoishi katika kisiwa hicho.
Wakazi wa kisiwa cha kusini mwa Italia wanasema wamefadhaishwa kutokana na msururu wa watu wanaowasili kwenye kisiwa chao kidogo.
Kisiwa hicho kwa miaka mingi kimekuwa kikijitahidi kudhibiti wanaoingia.
Lampedusa iko chini ya kilomita 160 kutoka Tunisia, na kukifanya kuwa kituo cha kwanza kwa wahamiaji wanaotafuta maisha bora Ulaya na kwingineko.
Forum