Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 00:16

Papa Francis asisitiza kwamba serikali za Ulaya lazima zifanye zaidi kuwahudumia  wahamiaji


 Papa Francis akiwa na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Mke wa Rais Brigitte Macron wakati wa hafla ya kuwaaga kwenye uwanja wa ndege wa Marseille. REUTERS. Septemba, 23, 2023
Papa Francis akiwa na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Mke wa Rais Brigitte Macron wakati wa hafla ya kuwaaga kwenye uwanja wa ndege wa Marseille. REUTERS. Septemba, 23, 2023

Akifunga mkutano wa maaskofu na vijana kutoka eneo kuzunguka bahari ya Mediterania katika mji wa bandari wa Ufaransa wa Marseille, aliongeza kuwa uhamiaji ni hali halisi ya nyakati zetu

Papa Francis siku ya Jumamosi alisisitiza ujumbe wake kwamba serikali za Ulaya lazima zifanye zaidi kuwahudumia wahamiaji wanaovuka bahari ya Mediterania, akisema wale wanaohatarisha maisha yao baharini hawavamii, bali wanataka kukaribishwa.

Akifunga mkutano wa maaskofu na vijana kutoka eneo kuzunguka bahari ya Mediterania katika mji wa bandari wa Ufaransa wa Marseille, aliongeza kuwa uhamiaji ni hali halisi ya nyakati zetu, mchakato unaohusisha mabara matatu kuzunguka Bahari ya Mediteranian na ambao lazima udhibitiwe kwa busara ikiwa ni pamoja na jibu la Ulaya.

Matamshi ya Papa yaliyotolewa mbele ya Rais Emmanuel Macron, ambaye serikali yake inapanga hatua kali zaidi za kudhibiti uhamiaji yanafuatia msisitizo wakati alipowasili Ufaransa siku ya Ijumaa kwamba watu ambao wako katika hatari ya kuzama wakati wakitelekezwa kwenye mawimbi lazima waokolewe.

Forum

XS
SM
MD
LG