"Kufikia Septemba 24, zaidi ya watu 2,500 walihesabiwa kuwa wamekufa au kupotea kwa mwaka 2023 peke yake," mkurugenzi wa ofisi ya UNHCR New York, Ruven Menikdiwela aliliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Idadi hiyo iliashiria kuwepo kwa ongezeko kubwa la zaidi ya wahamiaji 1,680 waliokufa au waliopotea katika kipindi kama hicho mwaka 2022.
"Maisha pia yanapotea ardhini, mbali na ya umma," aliongeza. Safari hiyo ya nchi kavu kutoka nchi za Afrika, kusini mwa Jangwa la Sahara, ambako wahamiaji wengi wanatokea, kwenda maeneo ya kuondokea katika mwambao wa Tunisia na Libya "imesalia kuwa mojawapo ya hatari zaidi duniani," alisema Menikdiwela.
Wahamiaji na wakimbizi "wanahatarisha maisha yao na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu katika kila hatua," alisema Menikdiwela.
Kwa jumla, watu wapatao 186,000 waliwasili kwa njia ya bahari kusini mwa Ulaya kuanzia Januari hadi Septemba 24, katika nchi za Italia, Ugiriki, Uhispania, Cyprus na Malta.
Wengi, zaidi ya watu 130,000, walifika Italia, na kuashiria ongezeko la asilimia 83 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2022.
Kuhusu sehemu za kuondokea, kati ya Januari na Agosti mwaka huu inakadiriwa kuwa zaidi ya wakimbizi na wahamiaji 102,000 walijaribu kuvuka bahari ya Mediterania kutoka Tunisia na 45,000 kutoka Libya.
Takriban watu 31,000 waliokolewa baharini au walizuiliwa na kushushwa Tunisia, na 10,600 nchini Libya, Menikdiwela alisema.
Forum