Kiongozi huyo anakutana na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta leo na wanatarajiwa kuzungumza juu ya jukumu la Kenya katika kuleta utulivu nchini Somalia, vita vyake dhidi ya ugaidi na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, kiutamaduni na kijeshi na Kenya.
Macron apokelewa kwa heshima kubwa
Rais Macron alipokelewa kwa heshima zote na Rais Uhuru Kenyatta alipowasili kwa ziara yake ya kwanza rasmi. Ziara hiyo ni ya kwanza kufanywa na kiongozi wa Ufaransa tangu Kenya kujinyakulia uhuru wake 1963.
Akiwa huko Nairobi kiongozi huyo atahudhuria mkutano wa baraza la mazingira la Umoja wa Mataifa linaloendelea kwa wakati huu na kukutana na viongozi wengine wa nchi za Afrika.
Kenya yaongoza kwa nishati mbadala
Ofisi ya Rais Macron inaeleza kwamba Kenya ndio nchi pekee ya Afrika iliyofikia lengo la kufanya nishati mbadala kuwa asilimia 75 ya mahitaji yake ya nishati, na hivyo watazungumzia ushirikiano katika nyanja za nishati.
Macron anafuatana na wakuu wa biashara kwa lengo la kuimarisha biashara kati ya nchi zao na kutia saini mikataba kadhaa ya biashara. Moja wapo ya mikataba hiyo ni mradi wa kiwanda cha kutengeneza magari elfu moja ya kampuni ya peugot mwisho wa mwaka 2019.
Wakati wa ziara hiyo makampuni ya Kifaransa yanasaini mikataba na Kenya yenye thamani ya Dola bilioni 2.26.
Lengo la ziara ya Macron
Wachambuzi wanasema ziara ya Macron inalengo la kuongeza ushawishi wa Ufaransa katika kanda hiyo ya Afrika pamoja na kushindana na ushawishi wa China ambao umepata nguvu katika nchi tatu anazotembelea nazo ni Djibuti, Ethopia na Kenya.
Kabla ya kuwasili Nairobi kiongozi huyo wa Ufaransa alikutana na mwenye kiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Mossa Faki Mahamat, Mjini Addis Ababa. .
Na akiwa hukoEthopia pia saini mkataba wa kwanza wa ushirikiano wa kijeshi na taifa hilo la Pembe ya Afrika, alitangaza msaada wa dola milioni 96 kwa ajili ya mradi huo,
Ufaransa, Kenya zasaini mikataba
Rais Macron aliosema : "Tumetia saini mkataba wa ushirikiano mpya wa ulinzi ambao utaweka mpango wa kuimarisha ushirikiano na kufiungua njia kwa msaada maalum kutoka ufarnsa kusaidia Ethopia kuunda kikosi chake cha majini."
Macron alimsifu Waziri Mkuu wa Ethopia Abiy Ahmed kwa kuleta mageuzi ya haraka na muhimu katika nchi yake
"Muna waziri mkuu aliyewajibika miezi michache tu baada ya kuchukua madaraka. Yuko katika kuleka mageuzi makubwa ya kuimarisha uchumi na maendceleo ya nchi hii na kufanya kila kitu kuleta maridhiano kati ya wananchi wake na kudumisha Amani katika kanda nzima," aliongeza.
Uhusiano wa Djibouti, Ufaransa
Kabla ya kwenda Ethiopia, Macron alifanya ziara nchini Djibouti ambayo ni moja ya nchi washirika wa Ufaransa wakuu katika bara la Afrika, akilieleza koloni lake la zamani kuwa mshirika muhimu wa kihistoria na kijeshi, na mlango muhimu kuingilia Pembe ya Afrika.
Ufaransa ina kambi yake kubwa kabisa ya kijeshi barani Afrika huko Djibouti sawa na Marekani na China.
Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC.