Utafiti huo unaeleza kiwango hicho kinaondowa matumaini kwamba mataifa yataweza kufikia malengo yaliowekwa na makubaliano ya Paris.
Ripoti hiyo imetolewa wakati wajumbe kutoka mataifa 190 wanakutana, mjini Katovich nchini Poland, katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa COPA24, unaolenga kutafuta njia za utekelezaji wa makubaliano hayo ya Paris.
Akizungumza kando ya mkutano huo mwandishi mshirikishi wa ripoti kuhusu mradi wa kimataifa wa kukabiliana na gesi za carbon– Corinne Le Quere, amesema kwamba China na Marekani zimeongeza kiwango cha uchafuzi unaotokana na gesi za carbon, huku kiwango cha hewa hiyo kikipungua barani Ulaya kinyume na ilivyotarajiwa.
Mashirika yasiyo ya kiserikali kwenye mkutano huo yameeleza kwamba kuna matumaini ya kufikia makubaliano ya utekelezaji wa mkataba wa Paris wa kupunguza hali ya joto duniani kwa kati ya nyuzi 1.5 hadi nyuzi 2 za Celsius.
Wajumbe wanasema ingawa kuna matumaini lakini kuna mvutano mkubwa katika majadiliano ambapo mataifa yanayoendelea yanataka uhakikisho kwamba ikiwa yatapunguza uchafuzi wa mazingira , mataifa yaliyoendelera kwa upande wao yatatekeleza ahadi zao za kugharimia mipango yao na athari zinazotokana na uchafuzi wa hewa. .