Akizungumza mbele ya Baraza Kuu la Bunge Michel alisema nchi yake itafanya juhudi zote katika kupambana na ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni
Watoto hao waliotekwa nyara ni wale waliozaliwa na wazazi wa kizungu na wa Kiafrika kati ya miaka 1940 na 50.
Watoto hao walichukuliwa kwa nguvu kutoka kwa mama zao wa Kikongo na kupelekwa Ubelgiji ambako walilelewa na familia mbali mbali pamoja na kanisa la Kikatholiki.
Kundi la waathiriwa 25 walihudhuria hotuba hiyo na mwishowe kubaki kimya kwa dakika moja kuwakumbuka wale waliopoteza maisha wakati wa ukatili huo.
Hii ni mara ya kwanza kwa ubelgiji kuomba radhi na kukiri kuwajibika kwake kwa ukatili uliotendwa katika miaka 80 ya utawala wake wa kikoloni nchini Congo.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC