Ubaguzi Marekani : Shinikizo la Gavana kujiuzulu laongezeka

Ralph Northam

Gavana wa Jimbo la Virginia anashinikizwa kujiuzulu baada ya kudhihirika kuwa aliweka picha ya ubaguzi wa rangi iliyokuwa imewekwa katika kitabu chake cha picha za kumbukumbu cha chuo cha udaktari zaidi ya miaka 30 iliyopita.

Ralph Northam ameomba msamaha Ijumaa kwa “ubaguzi na matusi” hayo katika mavazi ambayo yaliwekwa ndani ya kitabu hicho. Katika tamko alilolitoa kupitia picha ya video Northam amesema picha hiyo haiendani na yeye alivyo hivi leo.

“Siwezi kubadilisha maamuzi niliyofanya, wala kurekebisha madhara yaliyoletwa na tabia yangu ya wakati huo na hivi leo,” ameeleza zaidi.

“Lakini nakubali kuwajibika kwa vitendo vyangu vilivyopita, na niko tayari kufanya bidi kurejesha imani yenu kwangu.”

Kurasa ya kitabu hicho kinapicha ya mtu mwenye uso mweusi na mwengine amevaa mavazi ya kikundi cha ubaguzi wa rangi kilichokuwa na mavazi ya kutisha na kuficha utambulisho wao maarufu kama Ku Klux Klan garb.

Gavana ameeleza kuwa yeye ni moja wao katika hiyo picha lakini hajajitambulisha ni yupi kati yao.

Kikundi cha Wabunge Wamarekani Weusi na cha Baraza la Wawakilishi Weusi la Virginia vimemtaka mara moja ajiuzulu.

“Ralph Northam alikuwa na karne tatu za kujitambua zaidi lakini ni hivi sasa anakiri kitendo hiki cha ubaguzi wa rangi,” Kikundi cha Wabunge Weusi walitumwa ujumbe wa Twitter. “Kuomba msamaha hivi sasa haitoshi. Ni lazima ajiuzulu.”

Kikundi cha Baraza la Wawakilishi Wamarekani Weusi la Virginia limeposti tamko kupitia ujumbe wa Twitter ambao unasema kwa Northam: “ Tunashukuru sana yote ambayo amechangia katika maslahi yetu ya pamoja. Lakini kufuatia kile kilichodhihirika leo, ni wazi kuwa hawezi tena kututumikia kwa ufanisi kama Gavana. Ni wakati wa yeye kujiuzulu, ili Virginia ianze mchakato wa kuponya maradhi haya.”