Katika kuadhimisha siku hiyo Jumatano wananchi wa Afrika Kusini hujishughulisha na kazi za kujitolea.
Siku moja kabla ya maadhimisho hayo, Obama ambaye pia ni Rais wa kwanza mweusi alitoa hotuba ambayo inawezekana ilikuwa ni tamko lenye uzito mkubwa kuliko yote aliyotoa tangu amalize kipindi chake cha urais.
Kaitka hotuba yake siku hiyo ya kumbukumbu, inayofanyika kila mwaka kumuenzi Nelson Mandela, Obama alitoa sifa nzuri ya maendeleo na usawa yalioletwa na viongozi kama vile Marehemu Mandela, na kisha kulinganisha na kile alichokiita siasa za siku hizi za “ajabu na zisizoeleweka.”
“Mimi sio kwamba nawakatisha tamaa, lakini kwa ufupi naeleza ukweli ulivyo,” amesema. “Tizameni kila sehemu. Siasa za nguvu zinajidhihirisha ghafla, ambapo uchaguzi na demokrasia ya uongo zinaendelezwa katika sura hiyo, lakini wale walioko katika madaraka wanataka kukandamiza kila taasisi au mwenendo ambao unaipa maana demokrasia. Katika nchi za Magharibi, una vyama vya siasa vilivyobobea katika mrengo wa kulia ambavyo mara nyingi vimejikita katika majukwaa ya kulinda utaifa na kufunga mipaka, na pia wakijaribu kuficha ubaguzi uliowazi wa kitaifa.”
John Stremlau ni mhadhiri wa mahusiano ya kimataifa katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand. Amesema Obama ameeleza njia ya mbadala yenye mvuto yakufuatwa kinyume na ile ya siasa ya mrengo wa kulia inayoenea kwa kasi.
“Nilifikiria kuwa inatupa sote njia ya maendeleo mbadala kinyume na ile ya siasa za nguvu, nyenendo za kidikteta ambazo zinajitokeza katika nchi nyingi duniani, ikiwemo Marekani,” ameiambia VOA.
Na kitendo cha Barack Obama kumuenzi Mandela siku moja baada ya Trump kumsifia Putin huko Helsinki ilionyesha tofauti kubwa, japokuwa hilo lilikuwa linatarajiwa.
Stremlau alikuwa anaeleza juu ya mkutano wa wiki hii uliofanyika huko mji mkuu wa Finland kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Russia Vladimir Putin.
Japokuwa jina la Trump halikutajwa katika hotuba nzima ya dakika 90, Obama alitoa mifano mingi iliyokuwa wazi inamlenga Trump, mfano wa hili:
“Bahati mbaya siasa nyingi leo zinaelekea kukanusha dhana ile ile ya kuwa na lengo la ukweli,” Obama alisema. “Watu wanatengeneza mambo yao… Tunashuhudia kukosekana kwa aibu kati ya viongozi wa siasa ambapo wanakamatwa wakisema uongo na wanaongeza kusema uongo zaidi. Angalia wanasiasa siku zote wamekuwa wakisema uongo, lakini ilivyokuwa siku za nyuma wakikamatwa wanasema uongo watasema ah, bwana.’ Lakini hivi leo wanaendelea kusema uongo.