Trump aungana na viongozi wengine kuadhimisha ukombozi wa Ulaya

Malkia wa Uingereza Elizabeth II, akiwa na Prince wa Wales, katika picha ya pamoja na viongozi wa nchi za ushirika siku moja kabla ya maadhimisho ya 75 ya ukombozi wa Ulaya yanayojulikana kama D-Day, huko Portsmouth, Uingereza, June 5.

Rais wa Marekani Donald Trump ameungana na Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May, Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, Chansela wa Ujerumani Angela Merkel na viongozi wengine Jumanne kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya ukombozi wa Ulaya.

Ukombozi huo ulipatikana baada ya majeshi ya Ubaguzi ya Ujerumani ya Nazi kushindwa.

Sherehe hizo zilifanyika katika jiji la Portsmouth lilioko Kusini mwa Uingereza.

Sherehe hizo ziliadhimishwa kwa maonyesho mbalimbali ikiwemo muziki, simulizi za kihistoria, ambapo Trump alisoma maombi ambayo aliyasoma Rais wa zamani wa Marekani Franklin Roosevelt katika matangazo ya radio baada ya uvamizi wa majeshi ya Nazi mwaka 1944.

Ofisi ya May imetoa tamko kuainisha “ushirikiano wa kimataifa wa kihistoria “ uliyoshiriki katika kupeleka vikosi vya majeshi ya ardhini yaliyowasili eneo lote la eneo la English Channel huko Normandy, Ufaransa wakati majeshi ya ushirika yakifanya juhudi ya kulishinda jeshi la Nazi la Ujerumani.

“Wakati tukiungana kuwaenzi wale kwa ushujaa wao mkubwa na kujitoa muhanga katika maeneo ya pwani ya Normandy waliweza kubadilisha hatma ya Vita vya Pili vya Dunia, tutaendelea kuahidi kuwa hatutasahau wajibu wetu tulionao kwao,” May amesema.

“Mshikamano wao na azma yao katika kulinda uhuru wetu utaendelea kuwa ni somo kwetu sote.”

Malkia wa Uingereza Elizbeth alishiriki katika maadhimisho hayo ya kumbukumbu hiyo, ikiwemo ziara ya eneo waliozikwa mashujaa hao akifuatana na wapiganaji wa zamani na Trump.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.