Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 19:07

Trump kuzuru Uingereza mwezi Juni


Malkia Elizabeth wa pili na Donald Trump wakati rais huyo alipozurukasri ya Windsor mwaka wa 2018.
Malkia Elizabeth wa pili na Donald Trump wakati rais huyo alipozurukasri ya Windsor mwaka wa 2018.

Rais Donald Trump atazuru Uingereza mapema  mwezi Juni,  kwa mwaliko rasmi wa Malkia Elizabeth wa pili.

Taarifa iliyotolewa leo na Ikulu ya Washington, inaeleza kwamba Trump, akiandamana na mkewe Melania, wameukubali mwaliko wa Malkia Elizabeth, na kwamba watafanya ziara hiyo kutoka tarehe 3 had 5 mwezi Juni.

Taarifa hiyo inaeleza kwamba Trump na mkewe watahudhuria maadhimisho ya mika 75 ya uvamnizi uliofanywa na muungano wa kijeshi dhidi ya wapiganaji wa ki-Nazi, maarufu D-Day, uliopelekea ushindi wa muungano huo wakati wa vita vya pili vya dunia.

White House ilieleza Jumanne kwamba baadaye ya ziara hiyo ya kitaifa, Trump na ujumbe wake watazuru Ufaransa ambako watakutana na rais Emmanuel Macron.

Malkia Elizabeth II wa Uingereza.
Malkia Elizabeth II wa Uingereza.

Trump na Melania walikutana na Malkia Elizabeth kwa muda mfupi katika Kasri ya Windsor, wakati wa ziara ya rais huyo nchini Uingereza, iliyofanyika mwezi Julai mwaka uliopita.

XS
SM
MD
LG