Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 19:06

Trump kuanza ziara Uingereza Jumatatu


Rais Donald Trump na mkewe Melania Trump.
Rais Donald Trump na mkewe Melania Trump.

Rais Donald Trump na mkewe Melania Trump, wataanza ziara ya siku tatu nchini Uingereza Jumatatu.

Kwa mujibu wa ratiba rasmi kutoka White House, kati ya shughuli atakazokuwa nazo Rais Trump wakati wa ziara hiyo, ni kuhudhuria maadhimisho ya miaka 75 tangu uvamizi uliotekelezwa na muungano wa kijeshi wa nchi kadhaa, maarufu D-Day, uliofanyika mwezi mnamo mwaka wa 1944, wakati wa vita vya pili vya Dunia.

Takriban wanajeshi 156,000 wa Marekani , Uingereza na Ufaransa, walishiriki.

Hii si mara ya kwanza kwa Trump kuzuru Uingereaza kama rais lakini ndiyo ziara yake ya kwanza ya kitaifa.

Ziara rasmi ya kitaifa nchini Uingereza hufanyika baada ya kiongozi wa nchi au serikali kualikwa rasmi na Malkia Elizabeth wa pili.

Mwaliko ulitolewa kwa rais Trump muda mfupi tu baada ya rais huyo kula kiapo mwaka wa 2017, lakini masuala kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuhofia hali ya usalama, yamepelekea mipango ya ziara hiyo kutofaulu hadi sasa.

Ni marais 12 tu wa Marekani ambao wamezuru Uingereza, na ni wawili tu waliopata mwaliko rami wa kitaifa: George W Bush, mwaka wa 2003 na Barck Obama, aliyefanya ziara nchini humo mnamo mwaka wa 2011.

XS
SM
MD
LG