Kufutwa kazi kwa Waziri Gavin Williamson kumechochewa hasa ya ripoti iliyochapishwa mwezi Aprili na gazeti moja la Uingereza likisema kwamba waziri huyo aliiruhusu kampuni ya Huawei kuingia kwenye mtandao huo wa G5 katika mkutano wa usalama wa kitaifa.
Lakini Williamson alikanusha madai hayo alipoulizwa na wanahabari. Uingereza ambaye ni mshirika mkuu wa Marekani, imekuwa ikapata shinikizo la Marekani kuitenga kabisa Huawei kwenye mtandao huo wa G5 kwa hofu kwamba kampuni hiyo inaweza kutumia teknologia hiyo kwa kuifanyia ujasusi serikali ya China.
Uongozi wa shirika hilo la Huawei umekanusha kwamba unatumia mtandao wa G5 kwa sababu za ujasusi.
Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.